.LEO usiku mwingi tu, yaani saa 5:00 pale katika Uwanja wa Parc des Princes, Paris kutakuwa na mtikisiko. Vikosi viwili matata Manchester United ya Kocha Ole Gunnar Solskjaer na PSG ya Kocha Thomas Tuchel vitakuwa na kazi moja, kuonyeshana ubabe.
Uwanja unaonekana kuwainamia Manchester United mapema hasa kutokana na ukweli walichapwa 2-0 katika mechi ya kwanza huku wakati huu wakikabiliwa na majeruhi nane wa kikosi cha kwanza na nyota wao mkali Paul Pogba akiwa na kadi nyekundu, lakini msikie Solskjaer anachosema:
Tunafahamu itakuwa mechi ngumu, tuna kazi ya kupanda mlima, lakini kwenye soka lolote linaweza kutokea. Ninafahamu kuna majeruhi wengi, pia kuna wachezaji wengine wenye uwezo mkubwa.”
Ukiachana na Pogba wachezaji wengine wanane ambao watakosekana ni Ander Herrera, Nemanja Matic, Alexis Sanchez, Anthony Martial, Antonio Valencia, Mateo Darmian, Juan Mata na Jesse Lingard. Watu wengi wanaamini Man United ikipindua matokeo itakuwa ni moja kati ya miujiza ya soka.
Wakati timu hizi zilipokutana katika Uwanja wa Old Trafford mwezi uliopita mashabiki walitegemea ushindi kwa kikosi chochote kwa kuwa kikosi cha Kambi ya Old Trafford kilikuwa na kasi kubwa baada ya Solskjaer kuonyesha stamina kubwa tangu alipopokea timu Desemba mwaka jana. Vile vile suala la kukosekana kwa Neymar na Edison Cavani, liliwapa matumani mashabiki wa Man United. Lakini PSG walionyesha ukali kwa kupata mabao kutoka kwa Kimpembe na Kylian Mbappe.
Paris Saint Germain msimu huu inashtua kidogo, wamejikita kileleni wakiwa na pointi 71 wakiwa wameipita Lille inayoshika nafasi ya pili kwa pointi 17. Lille ina pointi 54. Bado PSG ina mechi moja mkononi. Wameshinda mechi 23 wametoka sare mara mbili na wamefungwa mechi moja tu. Kwa sasa wameshinda mechi saba mfululizo ikiwemo dhidi ya Man United mzunguko wa kwanza.
Kylian Mbappe amekuwa na kasi kubwa hasa baada ya kukosekana kwa Neymar na Edison Cavani. Amefunga mabao 29 pale PSG msimu huu na kusaidia mabao 12 kwenye michuano yote ya msimu huu.
Msikie kocha wa PSG Tuchel: “Kila kitu kipo sawa, tunaahidi kufanya vizuri. Nimewaambia wachezaji wasijidanganye kuona Pogba na nyota wengine wa Man United hawapo halafu wabweteke, wapambane mpaka hatua ya mwisho.”
MACHI 3, mwaka huu, Jumapili, Liverpool walisafiri hadi Goodison Park, kuvaana na majirani zao Everton FC, katika mechi ya Ligi kuu England, wakiwa na hitaji kubwa la kupata ushindi.
Ndio. Akili yako lazima itarudi katika usiku ule na kuiona sura ya Salah, ilivyoweka mikunjo. Taswira inayojijenga akilini ni namna Salah, alivyoghadhibika baada ya kukosa bao la wazi akiwa hatua chache, uso
kwa uso na kipa wa Everton, Jordan Pickford. Liverpool ilikuwa kileleni mwa msimamo pointi saba mbele dhidi ya mabingwa watetezi Manchester City. Kila mmoja alishaamini Liver ndio bingwa mtarajiwa, lakini sasa hali imebadilika. Liver ni kama kaishiwa nguvu.
Kwa sasa wako pointi moja nyuma ya Man City. Liver inaanza kuporomoka. Wameshaachia kiti, huku Man City wakiendeleza ubabe wao na kikosi chao chini ya Kocha mpenda mafanikio, Pep Guardiola.
Hata hivyo, usininukuu maneno yangu. Hii ni EPL, hakuna asiyeijua. Wengi wanajua ushindani ni timu mbili tu kwenye kuwania ubingwa lakini tukumbuke hii ni EPL, narudia tena hii ni EPL, lolote linaweza kutokea kwenye mechi zilizobaki. Wanaoielewa hii ligi wanasema ngoma bado mbichi sana.
Hata hivyo, pamoja na tofauti ya pointi moja kutokuwa tishio sana kwa jeshi jekundu la Jurgen Klopp, masahibu ya Liverpool, yanaonekana kumzunguka zaidi mtu mmoja; Mfalme wa soka la Misri, Mohamed Salah.
Kabla hatujapa jibu la swali hilo, ni busara kuendelea kumpa ‘mghala’ huyu sifa anayostahili. Ni haki yake. Salah, atabaki kuwa mmoja wa mastraika hatari katika kizazi hiki cha sasa. Hilo halina ubishi.
Salah hajafikia hatua aliyofikia Alexis Sanchez, hajachoka kiasi hicho. Lakini ukweli usiopingika, ameshindwa kuonyesha kiwango alichoonyesha msimu uliopita hasa anapokutana na timu kubwa. Katika mechi nane alizokutana na timu za top 6, ikiwemo ile dhidi ya Chelsea na Tottenham Hotspurs (hazijachezwa bado), amefanikiwa kufunga bao moja tu na asisti moja na zote ni katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Arsenal. Hiyo inamaanisha, mechi zilizobaki, alitoka kappa!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.