Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hakuonekana!

Ukiachana na mechi hizo za ‘Top Six’, takwimu za EPL, msimu huuzinaonesha, katika mchezo dhidi ya Wolves, Watford, West Ham United na Everton, stori ya Salah, ni ile ile. Hana makali tena, amekuwa nyoka wa kibisa.
 
Amefunga mabao matatu na asisti moja tu, katika mechi saba.

Mechizingine nne, ni kama hakuwepo uwanjani. Alifichwa mfukoni! Kukosa sumukatika mechi ya Merseyside Derby, ni jambo la kufikirisha sana. Watuwamenuna huko mitaani balaa!Kwa kifupi, kiwango cha Salah, kimeshuka ukilinganisha na msimu uliopita. Kwa nini? Jibu la swali hili, linaegemea mambo mengi.Kuna sababu kibao za kiwango kibovu kinachoonyeshwa na Mfalme huyo wa soka la Misri.
 
Presha

Baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika msimu wake wa kwanza Liverpool, na kutishia usalama wa kazi za mastraika wengi kwenye EPL, alianza msimu huu, akiwa na matumaini mengi.Presha kubwa ikitoka kwa mashabiki wake, ambao wameendelea kutarajiamakubwa kutoka katika miguu yake. Majukumu aliyokabidhiwa yanaonekana kumwelemea. Amechoka haraka, wakati ndio kwanza safari inaanza.
 
Bournemouth, kila mtu aliamini amerejesha makali yake ya awali. Kila mtu aliamini mabao yangeanza kutiririka kutoka katika mguu wa kushoto na kichwa chake, lakini haikuwa hivyo. Huo ukawa mwanzo wa kiwango kibovu kinachoshuhudiwa sasa hivi na mwisho wa makali yake.
 
Hajiamini

Hivi inaingiaje akilini, straika kama Salah, anaweza kukosa bao kama lile, akiwa uso kwa uso na kipa kama Pickford? Bao lile hata Meddie Kagere wa Simba au Jacque Tuyisenge wa Gor Mahia, hakuachi!
 
Ubunifu kwenye safu ya kiungo

Hapa ndipo mabao mengi ya Salah, msimu uliopita yalipopikiwa na kutengwa mezani. Kazi yake ilikuwa ni kutafuna tu, kitu ambacho msimu huu hakipo kabisa.Uwepo wa Philippe Coutinho, katika nusu ya kwanza ya msimu uliopita,ulichangia pakubwa, kupatikana kwa mabao mengi yaliyofungwa na miguuya Salah. Aina ya pasi alizokuwa anapata kutoka kwa Mbrazil yule,anazimiss sana.
 
[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
IMG_20160116_005127.jpeg
 
Back
Top Bottom