Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Meneja wa zamani wa Chelsea, Leicester na Fulham Claudio Ranieri, mwenye umri wa miaka 67, anakaribia kukamilisha taratibu za kuichukua klabu yake ya zamani Roma, baada ya upande wa ligi hiyo ya daraja la A kumfuta kazi Eusebio di Francesco. (Sky Sports)
 
Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri, mwenye umri wa miaka 51, amefichua kuwa mazungumzo kuhusu hatma yake ya siku zijazo yamesitishwa hadi mwishoni mwa msimu . (Mail)
 
Mshambuliaji wa Real Madrid Muhispania Isco, akiwa na umri wa miaka 26, ''amemkasirikia'' meneja wake Santiago Solari na ameelezea nia yake ya kuwasiliana na Manchester City. (Calciomercato, via Manchester Evening News)
 
Nahodha wa Real Madrid na Uhispania Sergio Ramos alikuwa na malumbano makali na rais wa klabu hiyo Florentino Perez kufuatia upande wa hiyo ya Championi kufungwa dhidi ya Ajax, huku Perez akitishia kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 . (Marca)
 
Meneja wa England Gareth Southgate anasisitiza kuwa hakuna mtizamo hasi dhidi ya wachezaji wanaochezea katika mataifa ya kigeni kama winga Jadon Sancho mwenye umri wa miaka 18- alivyofanya kwa timu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund. (Talksport)
 
Tottenham wamo katika harakati za kurejea White Hart Lane na Haringey Council huku wakitoa taarifa kwa maafisa wa usalama barabarani wakiwataka wahakikishe usalama wa barabarani kwa ajili ya majaribio ya matukio kuanzia mwishoni mwa juma lijalo . (Mail)
 
Liverpool itaangalia namna ya kupata mkopo utakaowasaidia kumchukua mchezaji wa Ligi ya Primia Harry Wilson msimu ujao - lakini kuwasili kwa Brendan Rodgers katika Leicester kunaweza kumaliza matumaini ya Foxes ya kusaini mkataba na winga huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye kwa sasa anacheza kwa deni katika Derby. (goal.com)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…