Kocha huyo Mhispaniola amesema hilo baada ya sasa kuwapo na uvumi ameshakubaliana na wababe hao wa Italia kwa ajili ya kwenda kujiunga na timu yao msimu ujao. Taarifa hizo zilidai kocha huyo amekubali ofa ya mkataba wa miaka minne kwenda kurithi mikoba ya Massimiliano Allegri huko Turin.
Akizungumza baada ya mchezo wa ushindi wa 3-1 iliyopata timu yake mbele ya Watford kwenye Ligi Kuu England, kocha huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich, Guardiola alizipuuza habari hizo za kuwa anajipanga kuachana na maisha ya Etihad ili akafanye kazi huko Serie A.
Ushindi huo wa juzi Jumamosi, shukrani kwa hat-trick ya Raheem Sterling imemfanya Guardiola kuendelea kushika usukani wa Ligi Kuu England na kukoleza mbio za kufukuzia ubingwa wa ligi hiyo dhidi ya Liverpool msimu huu.
MAURICIO Pochettino amewachenjia wachezaji wake akiwaambia hovyo kabisa baada ya kukubali kichapo kutoka kwa Southampton kwenye Ligi Kuu England juzi Jumamosi.
Kocha huyo wa Tottenham Hotspur, Pochettino amekiri kiwango cha timu yake kwa sasa kimeanza kumtia wasiwasi na huenda wakashindwa kumaliza ndani ya Top Four kwenye ligi hiyo msimu huu.
Spurs ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa straika wake, Harry Kane lakini Southampton, ambayo ni timu ya zamani ya Pochettino ilisawazisha kupitia kwa Yan Valery kabla ya James Ward-Prowse kuweka msumari wa pili kwa mpira wa adhabu aliopiga kutoka umbali wa mita 25.
Kwa hasira, Pochettino alisema: “Ni vigumu sana kuwaelewa hawa wachezaji kwa jinsi walivyoanza kucheza kipindi cha pili na kuwapa nafasi Southampton kuweza kutawala mchezo na kupata ushindi huo ambao haukutarajiwa.
Kichapo hicho kimeifanya Spurs sasa kujiweka kwenye nafasi ngumu na kusogelewa na vigogo wengine walipo nyuma yake kama Manchester United na Arsenal, ambazo usiku wa jumapili zilimenyana huko Emirates.
Kabla ya mechi hiyo ya Emirates, Spurs ilikuwa imeizidi Manchester United pointi tano tu, ikiizidi Arsenal pointi sita, hivyo yoyote atakayekuwa ameshinda kwenye mechi hiyo basi atapunguza pengo la pointi lililopo ama kubaki kuwa mbili au tatu.
MANCHESTER United imekubali kuwalipa Molde Pauni 6 milioni kwa kuwashukuru tu kwa kuwapa Ole Gunnar Solskjaer licha ya kwamba wangeweza kumbeba kocha huyo bure kabisa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.