Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kitu cha kwanza unachosema mara baada ya kuona bao kama lile ni kudhani kuwa labda mpira uliguswa njiani. Hata hivyo haukuguswa. Ulikuwa ni ubovu wa David de Gea. Sijui namna sahihi ya kuelezea hilo. Xhaka alipiga shuti kali. Alimuona vizuri David de Gea. Alipiga shuti kali lakini siwezi kumtetea kipa. Kipa alifanya ovyo,” alisema Neville.
 
Jinsi alivyojaribu kudaka alinishangaza. Alikwenda kushoto lakini hakuonekana kujishughulisha wakati mpira ulipokwenda kulia. Msimu huu hayupo katika ubora wake. Kumekuwa na kelele nyingi kuhusu mkataba wake. Inawezekana anasikia kelele nyingi masikioni mwake,” alisema Neville.
 
Naye staa wa zamani wa Liverpool na timu ya taifa ya England, Jamie Redknapp alikubaliana na Neville huku akisema “Lugha yake ya mwili inashangaza na nakubaliana na wewe Gary kwamba inabidi aongeze juhudi langoni.”
 
Staa mwingine wa zamani wa Liverpool, Graeme Souness alidai tatizo kubwa la United katika pambano hilo lilikuwa viungo wake watatu, Fred, Nemanja Matic na Paul Pogba ambao hawakuwa katika ubora wao na hawakuwa na kasi.
 
Haikuwa United ambayo tumeiona katika wiki za karibuni. Sababu kubwa ilikuwa eneo la kiungo. Hakukuwa na kasi. Fred, (Nemanja) Matic na (Paul) Pogba. Hawakumkaribia yeyote. Nimekuwa nikimkosoa Granit Xhaka mara nyingi lakini nadhani alikuwa bora sana. Alifanya kila kitu kwa usahihi. Tazama bao lake, Matic hakumkimbilia kabisa. United imepambana sana katika wiki za karibuni. Dhidi ya PSG walitumia sana nguvu lakini sio katika mechi hii,” alisema Souness.
 
Na sasa Arsenal inakamata nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa imeiondoa Man United ambayo kabla ya mechi ya juzi ilikuwa inashika nafasi hiyo. Wanasimama juu ya United kwa tofauti ya pointi mbili ikiwa na pointi 60 wakati United ina pointi 58.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…