Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Dietmar Hamann

Mmoja kti ya viungo bora wa mwisho mwisho wa Kijerumani ambao walikuwa wanacheza soka la shoka enzi zao. Dietmar Hamann maarufu kama Didi alikulia katika soka la vijana pale Allianz Arena. Mara nyingi alikuwa akicheza kama kiungo wa upande wa kulia.
 
Dietmar Hamann

Mmoja kti ya viungo bora wa mwisho mwisho wa Kijerumani ambao walikuwa wanacheza soka la shoka enzi zao. Dietmar Hamann maarufu kama Didi alikulia katika soka la vijana pale Allianz Arena. Mara nyingi alikuwa akicheza kama kiungo wa upande wa kulia.
 
Alitwaa mataji mawili ya Bundesliga baada ya kutua katika kikosi cha kwanza cha Bayern kisha akachukua na kombe la Europa. Mwaka 1998 alitua Ligi Kuu England na kutamba kiasi cha Liverpool kumnyatia katika msimu wake wa kwanza England.
 
Mwaka 1999 Liverpool walimchukua wakati Kocha Gerrard Houllier alipokuwa bosi wa timu hiyo. Hamman alitwaa mataji makubwa sita katika kipindi cha miaka sita aliyokaa Anfield ikiwemo mataji matatu kwa mpigo waliyotwaa mwaka 2001. Walitwaa kombe la Europa, FA na kombe la Ligi.
 
Xabi Alonso

Mtaalamu wa kupiga pasi za mbali kutoka Hispania. Xabi Alonso alikuwa mmoja kati ya wachezaji wa kwanza kujiunga na mapinduzi ya Kocha Rafa Benitez mwaka 2004 na moja kwa moja akageuka kipenzi cha mashabiki wa Anfield.
 
Alonso alikuwa nguzo kubwa katika ubingwa wa Ulaya wa Liverpool mwaka 2005 pale Istanbul huku akiacha sifa kubwa ya kutengeneza kombinesheni ya uhakika na staa kipenzi cha mashabiki wa Liverpool, Steven Gerrard.
 
Katika pambano la fainali dhidi ya AC Milan pale Istanbul, Alonso alifunga bao muhimu la kusawazisha huku miezi 12 baadaye akitwaa ubingwa wa FA. Alonso baadaye aliingia katika maelewano duni na Benitez na mwaka 2009 alihitimisha zama zake Anfiend kwa kuhamia Real Madrid ambayo nayo alitwaa nayo ubingwa wa Ulaya.
 
Markus Babbel

Aliwasili Anfield moja kwa moja akitokea klabu yake ya Bayern Munich ambayo aliichezea tangu akiwa mtoto. Aliwasili Anfield huku tayari akiwa mshindi. Alikuwa na matajhi matatu ya Bundesliga pamoja na kombe la Uefa.
 
Wakati huo alikuwa mmoja kati ya walinzi bora wa upande wa kulia na alipojiunga katika kikosi cha kocha, Gerard Houllier Julai 2000 alikuwa bora katika upande wake wa kulia huku Liverpool ikitwaa mataji matatu ya Europa, kombe la Ligi na FA mwaka 2001. Baadaye alikumbwa na ugonjwa wa ajabu ambao uliathiri miguu yake na alipopona hakucheza muda mrefu sana.
 
Pepe Reina

Aliponunua na Liverpool kutoka Villarreal katika dirisha kubwa la majira ya joto mwaka 2005, Reina alikuwa anachukuliwa kama kipa bora zaidi katika Ligi Kuu ya Hispania La Liga. Haikuwa uongo.
 
Baadaye akatua kwa mkopo Napoli na kisha kwenda Bayern Munich mwaka 2014 ambako muda mwingi aliutumia kuwa benchi kutokana na ubora wa kipa namba moja wa Bayern na timu ya taifa ya Ujerumani, Manuel Neuer. Hata hivyo, mpaka sasa Reina anachukuliwa kuwa mmoja kati ya makipa bora kutokea Anfield.
 
Christian Ziege

Katika orodha hii anakuwa mchezaji wa kwanza kuchezea Bayern Munich na Liverpool. Alianza kucheza soka akiwa golikipa kabla ya kuingia ndani ya uwanja na kuibuka kuwa miongoni mwa walinzi bora wa pembenio barani Ulaya.
 
Staa huyu wa kimataifa wa Ujerumani alitwaa mataji mawili ya Bundesliga na pia kutwaa kombe la Europa katika idadi ya mechi 185 alizocheza Allianz Arena. Baadaye alikwenda Italia kukipiga na AC Milan na kisha akatua Middlesbrough kabla ya kuhamia Liverpool mwaka 2000.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…