Wakati wa Mourinho, Pogba alivurugwa na kwenye akili yake kitu kilichokuwa kimejijenga ni kuachana na timu hiyo huku Juventus alipokuwa ikitajwa kuwa kwenye mpango wa kutaka kumrudisha kwenye kikosi chake.
Lakini baada ya Mourinho kuondoka staa huyo wa Les Bleus amebadili msimamo wake na amekuwa na uhusiano mzuri na kocha wa sasa Solskjaer, ambaye wamekuwa wakizungumza mambo yao mara kwa mara.
Kilichopo, msimu ujao Pogba anaweza kutajwa kuwa nahodha wa timu hiyo wakati kipindi cha Mourinho alivuliwa hadi unahodha msaidizi katika kikosi hicho. Chanzo cha kutoka huko Old Trafford kilifichua: βPogba amemwambia Ole hana mpango wa kuhama.
Wamekuwa na mazungumzo marefu sana. Akili yake sasa imekaa sawa baada ya kupita kwenye kipindi kile cha majaribu kutoka kwa Mourinho. Sasa mchezaji huyo hauzwi kwa pesa yoyote ile na hilo lipo wazi, Pogba atabaki klabuni na haendi kokote.β
SI unakumbuka Cristiano Ronaldo amepiga hat-trick dhidi ya Atletico Madrid ile Jumanne iliyopita, basi bana hizo bao tatu alizopiga kwenye mechi hiyo zimewaingizia Real Madrid mkwanja wa Pauni 540,000.
Staa huyo Mreno alifunga mara tatu kuisaidia Juventus kupindua matokeo ya kuchapwa 2-0 na Atletico Madrid katika mechi ya kwanza na hivyo kushinda 3-0 katika mechi ya marudiano na kutinga hatua ya robo fainali.
Iko hivi, kila timu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya inapata zawadi ya pesa, ikiwagawanywa kwa timu zote, lakini pesa nyingi zaidi zikienda kwa zile timu zinazoshiriki michuano hiyo na kufika mbali.
Kwa sababu Atletico ilimaliza juu ya Real Madrid msimu uliopita, basi wao pesa zao zitakuwa nyingi kuliko za Los Blancos kwenye michuano ya Ulaya msimu huu.
Real Madrid ianvuna kiasi hicho kwa sababu wakati timu zinafuzu kucheza michuano hiyo msimu uliopita kwenye ligi, staa huyo wa Kireno alikuwa kwenye kikosi cha Real Madrid.