Juventus ya msimu huo ilikuwa ina safu bora ya Ulinzi kwa maana ya BBC Bonucci, Brazagli, na Chiellin, walijikuta fainali wakipoteza mbele ya Real Madrid chini ya Cristiano Ronaldo.
Buffon, aliamini katika imani yake aondoke Juventus,akatafuta changamoto nyengine ametua Paris Saint Germain, wametupwa nje kwenye michuano hiyo hatua ya 16 bora na Manchester United.
Klabu ya Paris Saint-Germain wanatarajiwa kumpa ofa ya ongezeko la mwaka mmoja katika mkataba wake kocha Thomas Tuchel katika wiki kadhaa zijazo, kwa mujibu wa taarifa kutoka L'Equipe.
Kocha huyo wa Kijerumani ameiongoza PSG kuwa kileleni mwa msimamo kwa tofauti ya pointi 17 licha ya kwamba kutolewa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya raundi ya 16 bora dhidi ya Man United ni kasoro pekee.
Lakini PSG wameripotiwa kuwa na imani na kocha wao kwamba ataiongoza mbele zaidi klabu na Rais wa klabu Nasser Al-Khelaifi anajiamini kwamba Tuchel atakubali kusaini mkataba mpya.