Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

20190314_184053.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Arsenal na Leicester zote zina hamu ya kumsajili mchezaji wa Celtic na mlinzi wa Scotland Kieran Tierney, mwenye umri wa miaka 21. Leicester inamtaka Tierney aichukue nafasi ya mlinzi Ben Chilwell wakati wakitarajia maombi kuwasilishwa kwa mchezaji huyo. (Mirror)
 
Baada ya kumsajili mchezaji wa Brazil na Porto Eder Militao, Tayari Real imefikia kiwango cha mwisho kinachotakiwa cha wachezaji wasio raia wa Umoja wa Ulaya kwa mwaka ujao, na kufanya kuwa na uwezekano mkubwa kwa mchezaji wa Colombia, James Rodriguez kutojiunga nao punde tu mkataba wake wa miaka miwili utakapomalizika huko Bayern Munich. (Marca)
 
Real inataka kukusanya £128m katika mauzo ya wachezaji msimu huu wa joto na itaomba £42.7m kwa wachezaji Rodriguez na mchezaji wa kiungo cha kati wa Croatia Mateo Kovacic, kila mmoja, ambaye kwa sasa yuko Chelsea kwa mkopo. (El Confidencial)
 
Manchester United wamejiunga katika kutaka kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa PSG Adrien Rabiot, wa miaka 23. Raia huyo wa Ufaransa hana mkataba ifikapo msimu wa joto na tayari amezungumza na Barcelona, Arsenal, Chelsea na Tottenham. (Sun)
 
Aliyekuwa meneja wa Manchester United Jose Mourinho anasema hajahuzunishwa na kuteuliwa tena Zinedine Zidane huko Real Madrid. Mourinho, aliyehusishwa na kurudi katika timu hiyo kuu ya Uhispania amesema Zidane ndiye bora katika jukumu hilo. (El Chiringuito TV kupitia ESPN)
 
Back
Top Bottom