Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

.
FB_IMG_1552820779468.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahah anko bhana,siku nyingine nitakustua mapema ankoo,,tatzo una misamiati migumu hapo kwenye mkungu wa kunyorishia umeniacha hewani ankoo[emoji2][emoji2]
Nilikuwa kwa akina capitalpool kule kwa akina "iwe" mitaa ya kwenu nikapita mida mibovu...
Kunyorishia ni kuufunga mkuu juu ya carrier au samaki kuning'iniza kwenye side miror ya gari, kila mtu anaona na kutamanishwa
 
Hadi sasa taji kubwa ambalo hajawahi kubeba ni Kombe la Dunia tu, lakini mengine yote tayari, ikiwamo Ligi ya Mabingwa Ulaya alilobeba mara kibao. Huko kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ndiko Ronaldo anakoonyesha kwamba yeye ni balaa kubwa
 
Kwenye michuano ya Ulaya, Ronaldo ana timu zake anazozitesa kwenye michuano hiyo ya Ulaya, anapokutana nazo kwa kuzifunga mara nyingi. Hizi hapa ndio timu ambazo Ronaldo amezitesa kwa kuzifunga mara nyingi kwenye michuano ya Ulaya ikiwamo Ajax Amsterdam.
 
5. Ajax – mabao 7

Ajax waliwatupa nje Real Madrid kibabe kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu, lakini kwa bahati mbaya wamepangwa na Ronaldo kwenye mechi ya robo fainali, mchezaji ambaye amekuwa na kawaida ya kuwafunga sana. Kwenye hatua ya robo fainali, Wadachi hao wamepangwa kuwakabili Juventus, ambao ndiyo waliomwaajiri Ronaldo kwa sasa baada ya kumtoa huko Real Madrid. Huko nyuma, Ronaldo alikutana na Ajax kwenye mechi za makundi tu, ambapo kwenye msimu wa 2010/11, ambapo alifunga mabao kwenye mechi zote mbili, akifunga mara saba na kuasisti mara mbili.
 
4. Borussia Dortmund – mabao 7

Borussia Dortmund ilikuwa timu ngumu sana kwa Real Madrid. Lakini, Ronaldo wala hakuwa na ugumu wowote kwenye mechi alizokutana na Wajerumani hao kwenye michuano ya Ulaya, kwani ni miongoni mwa timu alizozifunga mara nyingi. Katika msimu wa 2012/13, Real Madrid ilikutana na Dortmund mara nne, Ronaldo akafunga bao moja katika mechi ya hatua zote za hatua ya makundi na kwenda kufunga jingine kwenye nusu fainali.
 
Msimu uliofuatia walikutana tena na Ronaldo alifunga bao kwenye ushindi wa 3-0 katika robo fainali. Katika msimu wa 2016/17 na 2017/18 walikutana tena kwenye hatua za makundi na Ronaldo amefunga mara nne katika mechi nne alizowakabili.
 
3. Atletico Madrid – mabao 7

Jumanne iliyopita, Atletico Madrid walisambaratishwa tena na Ronaldo, wakati alipowapiga mabao matatu na kuwasukuma nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye hatua ya 16 bora. Mabao hayo matatu yamemfanya Ronaldo kufikisha saba ambayo amewafunga Atletico katika mechi alizokutana nao kwenye michuano hiyo ya Ulaya.
 
Back
Top Bottom