Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Souness amesema matatizo ya Chelsea yanatokana na timu hiyo kukosa mizani sawa katika kiungo kilichoundwa na Jorginho, Ross Barkley na N'Golo Kante – ambao msimu huu wamefunga jumla ya magoli nane tu msimu huu.
 
Kipa David Ospina wa Arsenal ambaye yuko kwa mkopo Italia, alikimbizwa hospitalini baada ya kugongwa kichwani wakati akiitumikia Napoli katika mechi ya Serie A dhidi ya Udinese usiku wa kuamkia leo.
 
Kocha Thomas Tuchel amewasifu wachezaji wake baada ya PSG kuwafunga mahasimu wao Marseille katika mechi yao ya kwanza kwenye uwanja wa nyumbani tangu watolewe katika Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester United.
 
Goli la utangulizi la Kylian Mbappe lilisawazishwa na Valere Germain, lakini Angel Di Maria alifunga mara mbili na kuisaidia PSG kushinda 3-1 katika mechi hiyo ya mahasimu maarufu kama Le Classique na kupaa kwa tofauti ya pointi 20 kileleni mwa Ligue 1.
 
Wageni walicheza dakika 28 za mwisho wakiwa 10 baada ya Steve Mandanda kutolewa kwa kadi nyekundu kwa kushika mpira akiwa nje ya boksi. Di Maria akafunga kwa mpira wa adhabu iliyotinga moja kwa moja wavuni kutokana na kosa hilo la Mandanda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…