Gerard Pique vs Real Madrid
Beki wa kati wa Barcelona, Gerard Pique aliwahi kukiri huko nyuma kwamba siku zote amekuwa akitaka mambo yawaendee ovyo Real Madrid, hiyo ndio dua yake ya kila siku. Kwa chuki aliyokuwa nayo Pique kwa Real Madrid ni kwamba hata kama watacheza mechi dhidi ya jiwe, basi yeye atakuwa upande wa hilo jiwe. Kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2015, Pique hakutaka kuleta uzalendo sijui wa timu ya Hispania, yeye aliamua kuvaa jezi ya kipa wa Juventus kwa wakati huo, Gianluigi Buffon wakati timu walipowachapa Los Blancos kwenye mechi za michuano hiyo ya Ulaya.