Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Makocha wote moto Ulaya kwa sasa wapo kwenye ligi hiyo na kwamba ni miezi michache tu imepita tangu Jose Mourinho alipofutwa kazi, lakini kinyume cha hapo, basi makocha wote bora unaowafahamu wewe wapo kwenye ligi hiyo.
 
Jambo hilo litaleta vita kubwa, La Liga hawatakubali wanataka kurudisha makali yao na ndio maana kuna mastaa kibao kwenye Ligi Kuu England wanahusishwa na mpango wa kuhamia huko Hispania kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.
 
Lakini Los Blancos wana orodha nyingine ndefu ya wachezaji inaowasaka, akiwamo staa wa Chelsea, Eden Hazard, kiungo wa Tottenham, Christian Eriksen, kiungo wa Manchester United, Paul Pogba na fowadi wa Old Trafford, Marcus Rashford. Lakini Mane anasakwa pia na Barcelona
 
Kiungo wa Chelsea, N'Golo Kante naye yupo kwenye orodha. Wakati hilo la kuwahusisha mastaa wengi wa Ligi Kuu England wakitajwa kwamba wanaweza kutimkia Hispania mwishoni mwa msimu huu, vigogo wa England nao hawataki mchezo na kuhusishwa na mastaa kibao wa kutoka kwa La Liga, ikiwamo Isco, Toni Kroos kutoka Madrid, huku Philippe Coutinho na hata Ivan Rakitic wakitoka kwenye kikosi cha Barcelona huku taarifa hizo zikimhusu pia supastaa wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann anayesakwa huko Manchester kwa nguvu zote.
 
Kwa upepo ulivyo kwa sasa, La Liga imepania kurudi kwenye makali yake na ndio maana inalenga kuchota mastaa tupu wa kutoka England ambapo kwenye msako wao yupo pia fowadi wa Manchester City, Raheem Sterling.
Mastaa wa Spurs, Harry Kane na Dele Alli hawatajwi kwa sasa, lakini chochote kinaweza kutokea kwenye dirisha lijalo la usajili.
 
Bosi huyo wa zamani wa Manchester United na Chelsea alisema anatumia pia muda huu ambao hayupo kibaruani baada ya kufutwa kazi huko Old Trafford kupumzika kabla ya kurudi akiwa fiti kwelikweli kuwashika wapinzani wake.
 
Mourinho aliyejipachika mwenyewe jina la The Special One, alifutwa kazi Desemba mwaka jana huko Man United baada ya kushinda mechi mbili tu kati ya nane za mwisho na kibarua chake kilifika kikomo kufuatia kichapo cha 3-1 kutoka kwa mahasimu wao, Liverpool. Licha ya kuboronga huko Old Trafford ofa mbalimbali za kazi bado zinatumwa kwa Mreno huyo ambaye mwenyewe amesema anasubiri kazi sahihi anayoitaka.
 
Kazi ya ukocha ni spesho na naifurahia sana kazi hiyo. Nataka kurudi mwishoni mwa msimu huu, kuanzia Juni ili nianze msimu vyema. Nafahamu nisichokitaka na ndio maana nimekataa ofa tatu au nne hivi. Najua ninachokitaka na naamini nitakipata."
 
Mourinho amekuwa akihusishwa na Inter Milan pia, ambayo aliwahi kuinoa huko nyuma na kubeba mataji matatu makubwa mwaka 2010. Alihusishwa na Real Madrid, lakini wababe hao wa Bernabeu wameamua kumrudisha Zinedine Zidane kundini baada ya kumtimua Santiago Solari wiki iliyopita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…