Manchester United ina uwezo wa kumsaka winga wa Borussia Dortmund na Uingereza Jadon Sancho mwisho wa msimu huu kwa kuwa klabu yake ya zamani Manchester City haikuweka sheria yoyote ya kumzuia katika kandarasi yake baada ya kumuuza kwamba hafai kuwachezea wapinzani wao (Evening Standard)
Barcelona imepunguza moto wao wa kumtaka kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid na Ufaransa Antoine Griezmann kufuatia uvumi kwamba Manchester United itamsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Mirror)
Lazio inakaribia kufikia makubaliano ya kandarasi na beki wa Uhispania mwenye umri wa miaka 26 Alberto Moreno ambaye ataondoka Liverpool mwisho wa msimu huu baada ya kuhudumu kwa miaka mitano katika uwanja wa Anfield.. (Independent)
Barcelona inajiandaa kuwasilisha dau la £43m kumnunua mshambuliaji wa Serbia Luka Jovic na inatumai kuanza majadiliano na klabu ya Eintracht Frankfurt kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 katika kipindi cha wiki chache zijazo. (Guardian)
Beki wa kulia wa Paris Saint-Germain na Brazil Dani Alves, 35, amekanusha ripoti kwamba amekubali mkataba mpya na mabingwa hao wa ligi kuu ya Ufaransa . (Goal)
Kaimu mkufunzi wa klabu ya Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anawataka wachezaji Alexis Sanchez, beki wa Argentina Marcos Rojo, 29, na beki wa kulia wa Ecuado Antonio Valencia, 33, kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu. (Star)
Kiungo wa kati anayeichezea Chelsea kwa mkopo Mateo Kovacic, 24, yuko tayari kujiunga na klabu nyengine ya Uingereza badala ya kurudi katika klabu ya Real Madrid. (Marca)
Chelsea inaweza kumrudisha beki wa Uholanzi na Bournemouth Nathan Ake katika uwanja wa Stamford Bridge huku akivutia timu kama vile Napoli naTottenham. (De Telegraaf - via Caught Offside)
Arsenal itakabiliwa na ushindani mkali kutoka Bayern Munich katika harakati za kumsaka winga wa klabu ya Lille na Ivory Coast Nicolas Pepe, 23. (Bein Sports - via Mirror)
Mkufunzi wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa anataka kurudi katika ukufunzi mwisho wa msimu huu na kwamba tayari amekataa ofaa 'tatu' ama 'nne'. (Goal)
Ronaldo has been charged by UEFA last week after his provocative Simeone-like gesture following epic Juventus comeback, which has been defined as 'improper conduct'.
As is confirmed by UEFA, the Portuguese star will escape a Champions League ban which means he is available for both Ajax clashes in Champions League quarter-finals.
The verdict comes as no surprise, given Atleti boss Diego Simeone was handed the same punishment for celebrating in such a manner.