Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Beki wa Bayern Munich David Alaba, 26, amefichua kuwa alikuwa shabiki mkubwa wa Arsenal alipokuwa mtoto na kutoa ishara kwamba angependelea kuondoka katika uwanja wa Allianz Arena. (Bild via Daily Mail)
 
Winga wa West Ham Felipe Anderson, 25, ndio mchezaji mbadala anayelengwa na Real Madrid kwa dau la £65m iwapo klabu hiyo itashindwa kumvutia nyota wa Ubelgiji Eden hazard kutoka Chelsea (Sky Sports)
 
Inter iko tayari kushindana na Everton kumnunua kiungo wa kati wa Barcelona na Portugal Andre Gomes. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Goodison Park. (sport)
 
Rais wa klabu ya Bayern Munich Uli Hoeness anasema kuwa mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola husafiri ili kukutana na mmiliki wa klabu hiyo Sheikh Mansour na kumuonyesha kanda za video za wachezaji anaowalenga katika uhamisho ili kuweza kununua wachezaji hao. (goal)
 
Kwenye vita ya kumaliza ndani ya Top Four kumenoga zaidi. Tottenham Hotspur, Arsenal, Manchester United na Chelsea zote zina nafasi ya kuwapo kwenye orodha hiyo, ambayo inahitaji timu mbili tu baada ya Liverpool na Manchester City kuonekana kujichukulia nafasi mbili za mwanzo tayari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…