Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2019-03-23 Instagram(12).png
 
Kwa mfano mtu anaweza kuweka juhudi sana kwenye kazi yake au biashara yake, na ikamwezesha kuwa na kipato kikubwa sana, lakini akasahau kujenga mahusiano yake au familia yake. Pamoja na kuwa na fedha nyingi, maisha yake yanakuwa hayajakamilika kwa sababu maeneo mengine yanakuwa yameanguka.
 
Kadhalika mtu anaweza kuweka nguvu kubwa kwenye kujenga mahusiano yake na wengine, akawa na mahusiano bora sana, lakini fedha ikawa changamoto kubwa kwake, akawa kwenye madeni makubwa ambayo yanamkosesha uhuru wa maisha. Licha ya kuwa na mahusiano bora kwa mwenza wake, marafiki na hata familia, anakosa kuyafurahia maisha kila anapofikiria changamoto za kifedha alizonazo.
 
Katika juma hili la 12 la mwaka 2019, tunakwenda kujifunza kwa kina kutoka kitabu kinachoitwa

The Code of the Extraordinary Mind: 10 Unconventional Laws to Redefine Your Life and Succeed On Your Own Terms ambacho kimeandikwa na Vishen Lakhiani.
 
Katika kitabu hiki, Vishen anatuonesha jinsi ambavyo wale waliofanikiwa sana wanafikiri tofauti na watu wa kawaida na wanayatengeneza maisha wanayotaka wao na siyo kuishi maisha ya kuiga na ya mazoea, yale ya kufanya kile ambacho kila mtu anafanya.
 
Katika maeneo haya 12, kila eneo tutaangalia vitu vinne; ULIPO SASA, UNAKOTAKA KUFIKA, VIWANGO VYA KUJIWEKEA NA KITABU CHA KUSOMA.

Karibu tujifunze maeneo haya 12 kwa kina, ili uweze kuchukua hatua kuleta mlinganyo kamili kwenye maisha yako na kuwa na maisha bora na yenye mafanikio yaliyokamilika.
 
ENEO LA KWANZA; MAPENZI.

Hili ni eneo linalohusu mahusiano yako ya kimapenzi na mwenza wako. Ni eneo muhimu sana kwa sababu hili linagusa kila eneo la maisha yetu. Kama mahusiano yako ya kimapenzi yako vizuri basi maisha yako yanakuwa vizuri. Lakini kama eneo hili lina matatizo, hutaweza kutuliza akili yako kwenye jambo lolote.
 
ULIPO SASA; Tafakari pale ulipo sasa kwenye mahusiano yako ya kimapenzi, je umeoa au kuolewa au upo peke yako? Na je kwenye hali ya mahusiano uliyopo, unayafurahia? Unayaelezeaje mapenzi? Ni kitu gani unatoa na kipi unapokea kutoka kwenye mahusiano yako ya mapenzi? Je unaamini mapenzi yanaleta maumivu? Je upo tayari kumpenda kweli mwenzako na kumwonesha kwamba unampenda? Je unajiona ni mtu unayestahili kupendwa kweli? Jiulize na kujipa majibu ya maswali hayo na yatakupa picha ya pale ulipo sasa.
 
Back
Top Bottom