Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MAJALIWA ya Denis Suarez kwenye kikosi cha Arsenal anakocheza kwa mkopo yametajwa kuwa kwenye wasiwasi mkubwa kutokana na kutokuwapo na uwezekano wa Mhispaniola huyo kupata dili la kudumu la kuendelea kucheza kwenye kikosi hicho itakapofika mwisho wa msimu huu.
 
Suarez, 25, alinaswa na Arsenal akitokea Barcelona kwenye dirisha la Januari na kwamba hadi sasa amecheza dakika 67 tu huku kocha Unai Emery akionekana wazi kwamba bado hajafurahishwa na kiwango cha mchezaji huyo.
 
Junichi Inamoto - (Gamba Osaka, 2001)

Watu wengi walitaka kufahamu kulikoni wakati Arsenal ilipomsajili kwa mkopo kiungo wa Kijapani, Junichi Inamoto, ambaye baadaye walipaswa kumbeba jumla kwa ada ya Pauni 4 milioni.
 
Akiwa kinda, Inamoto alitua Arsenal akiwa kwenye moto kwelikweli akitamba kwenye J-League na hilo ndilo lililomvutia Arsene Wenger, ambaye alikuwa na ufahamu mzuri wa ligi ya Japan kwa sababu alikuwa katika timu ya Nagoya Grampus Eight. Lakini, kitu pekee ambacho kilikuwa na faida kwao Arsenal kwa kuipata huduma hiyo ya Inamoto ni kuongeza mauzo tu ya jezi zao huko Mashariki ya Mbali.
 
Inamoto aliichezea Arsenal mechi tatu tu, mbili kwenye Kombe la Ligi na moja kidogo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Leverkusen. Baadaye akatolewa kwa mkopo wa miaka miwili huko Fulham kabla ya kutimkia zake Uturuki, Ujerumani na Ufaransa. Kwa sasa anaripotiwa kuchezea timu ya Daraja la Tatu huko Japan, SC Sagamihara.
 
Mshambuliaji huyo wa Kibrazili alifunga mabao matatu tu katika mechi 24 alizocheza kwenye ligi, lakini alikuwa moto kwenye Kombe la Ligi akifunga mabao sita na kuwafanya Arsenal kufika fainali na kufungwa na Chelsea iliyokuwa chini ya Jose Mourinho.
 
Kumbukumbu zake nzuri kwenye kikosi kile zinakuja kwenye robo fainali ya Kombe la Ligi ambapo alifunga hat-trick dhidi ya Liverpool wakati Arsenal ilipoibuka na ushindi wa 6-3 uwanjani Anfield. Baptista alirudi zake Real Madrid na hakuonekana tena kwenye Ligi Kuu England huku mara ya mwisho akionekana kwenye klabu ya Cluj ya Romania.
 
Yossi Benayoun - (Chelsea, 2011)

Uhamisho wa kushtukiza iliyofanya Arsenal kwa kumbeba kwa mkopo Muisraeli Yossi Benayoun kutoka Chelsea. Licha ya kucheza mechi 19 tu za Ligi Kuu England, Yossi ambaye kipindi hicho alikuwa na miaka 31 alikuwa na mchango mkubwa kwa Arsenal.
 
Kiungo huyo alianzishwa kwenye mechi muhimu dhidi ya Tottenham , Liverpool na Manchester City na alifunga pia mabao na kusaidia timu hiyo kukamatia nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya mahasimu wao Spurs. Benayoun alirudi Chelsea mwishoni mwa msimu na kutolewa tena kwa mkopo kwenda West Ham.
 
Thierry Henry - (New York Red Bulls, 2012)

Kinara wa mabao wa muda wote Arsenal, Thierry Henry alirudi kucheza kwa mkopo wa miezi miwili akitokea Marekani kwenye kikosi cha New York Red Bulls. Msimu wa Ligi Kuu England ulikuwa umefika mwisho, hivyo Henry alirudi Arsenal kuja kuziba pengo la Marouane Chamakh na Gervinho waliokuwa wamerudi Afrika kucheza kwenye Afcon 2012. Walau Henry alikuwa na wakati mzuri alipocheza kwa mkopo akiifungia Arsenal bao la ushindi kwenye mechi ya raundi ya tatu ya Kombe la FA dhidi ya Leeds United, ambapo The Gunners walishinda 1-0.
 
Emiliano Viviano - (Palermo, 2013)

Emiliano nani? Yawezekana wengi wakauliza swali hilo. Katika siku ambayo Arsenal ilifanya usajili wa Mesut Ozil uliovunja rekodi ya klabu kwenye uhamisho, wababe hao wa Emirates walimnasa pia kipa Emiliano Viviano kwa mkopo kutoka Palermo ya Serie B huko Italia. Lakini, hakucheza mechi yoyote akiwa Arsenal akikosa namba mbele ya Wapolandi wawili, Wojciech Szczesny na Lukasz Fabianksi.

Mechi aliyocheza kwenye timu hiyo ni huko ya kikosi cha U21, ambapo alipigwa bao tano wakati walipochapwa 5-1 na Sunderland.
 
Kim Kallstrom - (Spartak Moscow, 2014)

Katika dirisha la usajili wa Januari 2014, Arsenal walikwenda Spartak Moscow kumsajili Kim Kallstrom kwa mkopo baada ya wakali wake Jack Wilshere na Aaron Ramsey kuwa majeruhi na Mathieu Flamini alikuwa na adhabu. Wenger aliona suluhu ni kumnasa kwa mkopo Kallstrom, wakati huo akiwa na miaka 31.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…