Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wanaweza kuwa walikuwa na ligi maarufu zaidi duniani na wachezaji wazuri kabisa wa kimataifa katika ngazi ya klabu, lakini kwenye suala la kimataifa, Timu ya Taifa ya England – Three Lions, walikuwa wabovu.
 
Ubovu huo ulidhihirika kwenye mashindano mengi, yakiwamo yale ya Ulaya na fainali za Kombe la Dunia. Ilikuwa mbinde kuvuka hatua ya robo fainali na walikuwa wakifungwa na timu za mataifa makubwa na yale madogo kadhalika, hadi ikawa aibu kwa Waingereza walioishia kutembea vichwa chini.
 
Walianza wale wa timu za vijana wadogo na sasa kaka zao wanafuata kufanya vyema, japokuwa inajulikana kwamba kwa hakika kuna ugumu katika kufanya uendelevu kwenye hali waliyoianzisha sasa, maana Waingereza wameanza kutamba kweli huko mitaani juu ya vijana wao – Three Lions.
 
Hali ya hewa ilianza kubadilika kwenye fainali zilizopita za Kombe la Dunia nchini Urusi, ambapo walifyeka timu moja baada ya nyingine kwenye hatua za makundi, wakachupa hadi robo fainali, vihoro vikaanza lakini wakavuka vile vile hadi nusu fainali, wakatolewa katika muda wa ziada na Croatia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…