Alifunga bao kwenye mechi ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Moldova, huku mabao mengine kwenye mechi hiyo yalifungwa na Antoine Griezmann, Raphael Varane na Olivier Giroud. Jumatatu Les Bleus walitarajia kukipiga dhidi ya Iceland.
KOCHA wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps ni kama anamwambia kijanja supastaa wake Antoine Griezmann ahame kwenye kikosi cha Atletico Madrid.
Kinachoelezwa ni kwamba fowadi huyo anaweza kuachana na wababe hao wa Hispania kwenye dirisha lijalo la usajili na kinachoelezwa ni mchezaji huyo anaweza kuibukia huko Manchester United huku Paris Saint-Germain nao wakihitaji saini yake.
Mwaka jana kwenye uhamisho wa majira ya kiangazi Griezmann aligoma kuhamia Barcelona, huku mwaka mmoja kabla alishindwa kwenda Man United kwa sababu wakati huo timu yake Atletico ilikuwa imefungiwa kufanya usajili.
Lakini, sasa wakati dirisha la usajili wa majira ya kiangazi halipo mbali sana kufunguliwa, Griezmann yupo kwenye rada za vigogo kadhaa wakiwamo Barca, Man United na mabingwa wa Ufaransa, PSG.
Kwenye mkataba wa mchezaji huyo kumewekwa kipengele kinachohitaji kulipwa Euro 120 milioni kwa timu itakayohitaji kumsajili mshambuliaji huyo kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa wachezaji huko Ulaya.
Kocha Deschamps ni kama anamchochea mshambuliaji huyo aondoke baada ya kusema: “Kutokana na kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Atletico imemsababisha msongo mkubwa sana wa kimawazo Griezmann. Pengine sasa ni wakati wake wa kufanya uamuzi. Hilo litamhusu mwenyewe.”
.DALILI si nzuri kwa mchezaji anayeitwa Naby Keita. Upepo hauvumi vema pale Anfield. Alitinga katika kikosi cha Liverpool kwa mbwembwe lakini kuna uvumi huenda akaruhusiwa kuondoka katika dirisha kubwa lijalo.
Keita staa wa kimataifa wa Guinea alisubiriwa kwa mbwembwe Anfield kwa miezi 12 baada ya Liverpool kukamilisha uhamisho huo katika dirisha kubwa la majira ya joto mwaka 2017 lakini akasubiri mpaka dirisha la mwaka 2018 kujiunga rasmi na wababe hao.
Liverpool ililipa Pauni 52 milioni kwenda kwa RB Leipzig lakini staa huyo ameshindwa kuonyesha makali yake kama ilivyotarajiwa ambapo ilidhaniwa kuwa angeziba vema pengo la kiungo wa kimataifa wa Brazil, Philippe Coutinho aliyeuzwa kwenda Barcelona Januari mwaka jana.
Keita 24, ameshindwa kufunga bao lolote mpaka sasa katika mechi 27 alizocheza huku Kocha Jurgen Klopp akimuweka kama chaguo la nne mbele ya James Milner, Fabinho na Giorginio Wijnaldum ambao wamekuwa wakicheza mara kwa mara.
Ndani ya misimu miwili akiwa na Leipzig Keita alifunga mabao 14 katika mechi 58 za Ligi Kuu ya Ujerumani lakini ameshindwa kurudia kiwango hicho cha ufungaji huku pia rekodi yake ya upikaji mabao ikionekana kutokwenda sawa.
Klabu mbili kubwa za Bayern Munich na Borussia Dortmund ambazo zilimtaka Keita wakati akiwa Ujerumani lakini zikapigwa bao na Liverpool inasemekana zinamtaka tena staa huyo katika dirisha kubwa lijalo kama Liverpool ikiamua kumuuza.
Liverpool inatazamia kupata hasara hadi ya Pauni 10 milioni kwa Keita ambaye tayari wawakilishi wake wanatajwa kuwa tayari kuzungumza na klabu hizo mbili za Bundesliga kwa ajili ya kumrudisha Ujerumani ambako alijenga jina kubwa.
Liverpool imekuwa ikihusishwa na viungo mbalimbali barani Ulaya huku ikionekana kuwa bado Kocha Klopp ameshindwa kuziba pengo la Coutinho ambaye alikuwa anafunga zaidi pamoja na kutengeneza mabao.
Kumekuwa na mjadala kuhusu kiwango cha Keita huku wengine wakiamini anahitaji muda wa kuzoea Ligi Kuu ya England lakini baadhi ya mashabiki wanaamini Liverpool ‘imepigwa’ na Leipzig baada ya kutoa pesa nyingi kwa mchezaji ambaye ameshindwa kuonyesha kiwango.
Keita aliingia pamoja na kiungo wa kimataifa wa Brazil, Fabinho ambaye alianza kwa kusuasua katika kikosi cha Klopp lakini kadiri siku zilivyosonga mbele Fabinho alipewa nafasi zaidi na kwa sasa anaonekana kuwa mchezaji wa kudumu mbele ya Keita.
Wakati hatima ya Keita ikianza kutoeleweka inadaiwa Klabu ya Juventus ipo tayari kumtumia staa wake Paulo Dybala kama chambo cha kumnasa nyota wa Liverpool, Mohamed Salah katika uhamisho ambao unakadiriwa kufikia Pauni 175 milioni.
Dybala anataka kuondoka Italia baada ya nyota yake kufifia tangu kuwasili kwa Cristiano Ronaldo na Juventus inataka kutumia nafasi hiyo kujaribu kuishawishi Liverpool iwape Dybala na pesa kwa ajili ya kumnasa Salah.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.