Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Wembley yote ilisimama baada ya kipenga cha mwisho, kwenye mechi dhidi ya Jamhuri ya Czech, ambapo Waingereza waliwasasambua kwa mabao 5-0, tena ikizingatiwa kwamba Czech si taifa dogo kisoka. Wapenda soka wa hapa wakasema kwamba huu ni mwanzo wa kitu cha kipekee kwenye soka ya England.