Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Thank God for the storms in your life...
449014405_365308.jpeg
 
WAKATI Waingereza wakileta mapozi na kudhamiria kujitoa katika Umoja wa Ulaya, huku moja ya sababu kuu zikiwa ni kutaka kudhibiti idadi ya wageni, timu ya taifa ya England imeanza kampeni za kufuzu kwa fainali za Euro 2020 ikiundwa na kikosi kilichojaa watoto wa wahamiaji.
 
“Watu huhama kutoka nchi moja kwenda nyingine kwa sababu mbalimbali,” alisema kocha wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate. “Kwenye timu za vijana, zaidi ya nusu ya wachezaji vijana wana uraia wa nchi mbili au wanaweza kuchezea nchi mbili. Hiki ni kitu cha asili duniani.”
 
Nyota wa West Ham, Declan Rice, ndiye mchezaji mpya zaidi kuhamishia uraia wake England akiwa tayari alishachezea timu ya taifa ya wakubwa ya Ireland katika mechi tatu. Ameruhusiwa kuchagua kuchezea England sasa kwa kuwa mechi alizocheza hazikuwa za kimashindano.
 
Back
Top Bottom