KINDA WA JUVENTUS AMKANA BABA YAKE. : Jina la Moise Keani limeshika vichwa vingi vya habari siku za hivi karibuni kutokana na kiwango maridhawa. : Baba yake Moise alijitokeza hivi majuzi na kueleza kuwa hapo awali Juventus walimuabidi matrekta kwa ajili ya kilimo. Lakini Juventus wakaja kumkana na kumwambia hawana bajeti hiyo. : Baada ya Moise kusikia hayo, jana ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusema "Matrekta? Mbona mimi sijui hayo mambo? Nimefika hapa nilipo kwa msaada wa mama. Sema kila kitu lakini usimsahau anayekupa chakula" Moise : Kauli hii inaonesha wazi kuwa Moise hana mahusiano mazuri na baba yake ndio maana ameweka hadharani kuwa makubaliano hayo ni batili na hayatambui. : Hata hivyo baba yake amesema kuwa mama yake Moise anamrubuni mwanae watimkie England. : "Mahusiano yangu na Juventus yamepungua, na mama yake anamlazimisha waende England. Hali hii imesababisha hata Juventus waninyime tiketi za bure uwanjani." Baba yake Moise