Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Muhammad Buhari.
Buhari kabla ya urais alionao sasa aliwahi kuitawala Nigeria kuanzia 31 Desemba 1983 mpaka August 27 1985.
Aliingia madarakani kimabavu bàada kuondoa utawala wa kiraia uliokua chini ya rais Shehu Shagali, kwa mapinduzi yasiyokuwa ya umwagaji damu.
Utawala wa kijeshi wa Meja Jenerali Muhammadu Buhari ulijaa mateso kwa wanaigeria.
Katika tukio furani Buhari alimkamata mfanyabiashara mmoja wa Nigeria jijini London kwa msaada wa majasusi wa Mosad, akadungwa sindano ya usingizi na kujaribu kumsafirisha kwenye jeneza kama maiti. Hata hivyo jaribio hilo lilizimwa na vikosi vya usalama vya Uingereza kwenye uwanja wa ndege wa Heathrow.
Tukio hilo lisisimua sana Dunia wakati huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…