Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 26 nchini Ureno, amejifungua mtoto wa kiume siku ya Alhamisi licha ya kutangazwa kuwa ni mfu toka mwezi Disemba mwaka jana.
Mtoto huyo aliyepewa jina la Salvador, amezaliwa baada ya kukua kwa wiki 32 tumboni mwa mama yake na sasa yupo chini ya uangalizi kwenye hospitali ya watoto.
Shambulio lililochukua uhai wake lilimpata akiwa na mimba ya wiki 19, hali iliyomfanya kupoteza fahamu. Siku chache akiwa chumba cha wagonjwa mahututi hali ilizidi kuwa mbaya na akatangazwa kuwa ‘mfu wa ubongo’ Disemba 26. Madaktari wakamuwekea mashine ya kusaidia kupumua ili mtoto tumboni aweze kuishi. Mashine hiyo iliwekwa kwa siku 56.
Sheria ya kutoa viungo yaamua ‘kesi’ hii
Madaktari wanasema malengo yalikuwa ni kusubiri mpaka Ijumaa ambapo ujauzito huo ungefikisha wiki 32, lakini mfumo wa hewa wa mama huyo uliharibika ghafla na kulazimisha upasuaji ufanyike Alhamisi ili mtoto atolewe.
General Sani Abacha enzi za utawala wake wa kibabe, alimuua mwanaharakati wa Mazingira Kenule Beeson "Ken" Saro Wiwa. Pichani chini. Saro-wiwa aliuwawa alipojaribu kupinga kwa njia ya harakati kuchimbwa mafuta kwenye
Delta ya Niger. "Niger Delta" kwa sababu ya uharibifu wa mazingira
Mkuu wa kitengo cha maadili cha hospitali hiyo, Filipe Almeida, ameelezea kuwa maamuzi ya kumuacha mtoto aendelee kukuwa kwenye tumbo la mama yake yalifikiwa kwa pamoja na familia ya mama huyo, kwa sababu katika uhai wake hakuwahi kipinga kwa maandishi sheria ya kutoa viungo vyake baaa ya kufariki.
Kuwa mtoaji wa viungo si tu kuwa na nafasi ya kutoa ini au mapafu, lakini pia inahusu kuwa na uwezo wa kujitoa ili mtoto wako aishi,” Almeida ameuambia mtandao wa Observador.
Hata hivyo mama wa Sequeira, Bi Maria de Fátima Branco, ameiambia televisheni moja ya Ureno kuwa alimuaga binti yake Disemba 26, na uamuzi wa kumuacha mtoto huyo azaliwe umefikiwa baada ya baba yake, Bruno, amekuwa akitaka kuwa baba kwa muda sasa.