MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,775
- 71,893
Mkuu nimeisoma na nimesikitika kuona Waziri hajui bajeti ya kukimbiza mwenge ndani ya mwaka. Lakini mbali na kufungua miradi mbalimbali mimi sijaona faida zozote za kukimbiza mwenge.Sasa Mkuu kama watu wananufaika na wizi wa kufa mtu kupitia Mwenge unadhani watakuwa tayari kufuta mbio hizo na hivyo kufuta shamba lao wanalovuna kila mwaka?
![]()
Kama ni kuhamasisha kujitegemea nadhani hilo limekaa kifalsafa zaidi na msingi wake ni Azimio la Arusha na siyo mwenge. Bahati mbaya sana Azimio la Arusha halipo.
Lakini kikubwa zaidi ni kwamba mwenge wa Uhuru ulianza kukimbizwa hata kabla ya kuzaliwa kwa Azimio la Arusha lililoleta falsafa ya ujamaa na kujitegemea mwaka 1967: Captain Nyirenda alikimbiza mwenye hadi Kilimanjaro mwaka 1961 na lengo lilikuwa siyo kujitegemea.
Nakumbuka utotoni nilitolewa darasani kisa kwenda kukimbiza mwenge huku tukiambiwa na walimu tuimbe na tushangilie kama watu waliopagawa: Mpaka leo hii miaka imepita sijawahi kupata mantiki ya sisi kucheza huku tukiuzunguka gari la mwenge.