Ikiwa imefufuliwa na Ole Gunnar Solskjaer, United imeweza kurejea katika kinyang'anyiro cha nafasi nne za juu baada ya kuwa chini kwa tofauti ya pointi 11 wakati kocha Jose Mourinho alipotimuliwa mwezi Desemba.
Mechi za ugenini dhidi ya Wolves, ambayo hivi karibuni iliiondoa United katika Kombe la FA, na Everton hazitakuwa rahisi wakati Solskjaer akitafakari jinsi ya kuivaa Barcelona katika mechi za robo fainali.
Kumalizia msimu kwa mechi dhidi ya Huddersfield na Cardiff kutakuwa na unafuu lakini United inatakiwa ihakikishe kuwa inafikia mechi hizo ikiwa na matumaini hai ya kuwa moja ya timu nne za juu.
Ikiwa nyuma tya timu nne za juu kwa tofauti ya pointi nne, Chelsea iliyo katika nafasi ya sita haina nafasi ya kufanya makosa mwishoni mwa msimu wa kwanza wa kocha maurizio Sarri uliokuwa mbovu kwake.
Kutwaa Kombe la Europa kunaweza kuwa nafasi bora kwa Chelsea kucheza Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, kwa kuangalia kuwa watavaana na Liverpool na Manchester United katika mechi za Ligi Kuu.
Kabla ya mechi hizo, Chelsea itakuwa na mechi ambazo ni lazima ishinde dhidi ya Cardiff, Brighton na West Ham, huku Burnley, Watford na Leicester zikiwa katika wiki za mwisho.
* Viumbe hawa wakijihakikishia akiba ya chakula katika himaya zao, basi hufanya sherehe na sherehe zao huwa na ufanano na sherehe za binadamu, hucheza, hufurahi, hufanya ngono na ugomvi huzuka pia wakati huo watoto wote hufichwa ndani ya nyumba.