Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

3. Luis Suarez – miaka 32, mabao 18

Lionel Messi ameendelea kuwa mtambo wa mabao kwenye kikosi cha Barcelona katika La Liga baada ya kufunga mabao 31 na kuasisti mara 12 kwenye ligi hiyo msimu huu. Lakini, pamoja naye, Luis Suarez pia amekuwa kwenye ubora mkubwa wa kufunga mabao. Kwa mabao, nyuma ya Messi yupo Suarez licha ya kuwa na umri wa miaka 32.
 
2. Cristiano Ronaldo – miaka 34, mabao 19

Cristiano Ronaldo aliandika rekodi nyingi sana zinazohusu namba za mabao wakati alipokuwa huko Santiago Bernabeu kabla ya sasa kuhamishia makali yake kwenye kikosi cha Juventus. Huko kwenye Serie A, supastaa huyo wa Kireno ameendelea kuwatesa makipa bila ya kujali kwamba umri wake umekimbia kwa kasi ya ajabu.
 
Ronaldo kwa sasa umri wake ni miaka 34, lakini hajafunga breki katika kutupia mipira kwenye nyavu. Amefunga mabao 19 na kuasisti mara 10 katika mechi zisizozidi 26 alizocheza kwenye Serie A msimu huu ambao ni wa kwanza kwake baada ya kujiunga na wababe Juventus akitokea Real Madrid mwaka jana katika kipindi cha uhamisho wa majira ya kiangazi.
 
1. Fabio Quagliarella – miaka 36, mabao 21

Sampdoria wana kila sababu ya kujivunia msimu huu kutokana na kiwango bora kabisa wanachokipata kutoka kwa mchezaji wao Fabio Quagliarella. Staa huyo mwenye umri wa miaka 36 ameamua kuwaonyesha vijana wadogo namna mabao yanavyofungwa kwenye Serie A kutokana na kufunga mabao 21 na kuasisti mara saba kwenye ligi hiyo.
 
Quagliarella amecheza mechi 28 za ligi msimu huu, akikosa moja tu jambo linalofichua kwamba umri kuwa mkubwa halijawahi kumzuia kwenye mipango yake ya kuitumikia vyema Sampdoria msimu huu na hivyo kuwa sehemu muhimu ya kikosi hicho katika kusaidia kupata pointi muhimu.
 
Kwenye riziki hapakosi fitina. Ole Gunnar Solskjaer amepewa kazi ya kudumu pale Manchester United lakini kuna watu wameanza kupenyeza maneno ya chinichini kwamba United imefanya makosa kumpa kibarua cha kudumu staa wake huyo wa zamani.
 
Juzi Solskjaer alianza rasmi kuwa kocha wa kudumu wa United katika pambano dhidi ya Watford pale Old Trafford lakini staa wa zamani wa Tottenham na Timu ya Taifa ya England, Jermaine Jenas amedai United huenda imefanya makosa.
 
Jenas amedai United itajuta kutompa kazi ya kudumu Kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino huku akidai rekodi za Solskjaer katika klabu zake mbili alizopita zinatia wasiwasi licha ya kuanza vema kazi yake United.
 
Nilikuwa na furaha kuona Manchester United imemthibitisha Ole Gunnar Solskjaer kuwa kocha wake, lakini nadhani ingemteua Mauricio Pochettino. Ukiangalia kwa jumla na mambo ambayo inataka kufanikiwa, rekodi yake na hadhi yake klabuni vilimfanya awe mgombea wa nafasi hiyo,” anasema Jenas.
 
Msinikariri vibaya. Solskjaer amefanya kazi nzuri sana, amerudisha historia ya klabu hiyo na alama ya klabu hiyo huku kiwango uwanjani kikiongezeka. Katika mbinu za uwanjani alifanya vizuri katika mechi kama vile dhidi ya Tottenham, dhidi ya Arsenal katika Kombe la FA na PSG katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya. Kwa vigezo hivi anastahili.”
 
Hata hivyo, hakuwa chaguo la kwanza mwezi Desemba na nashangaa kwanini klabu haikuchukua maamuzi magumu kubakia katika mpango wake wa awali. Labda ilihofia huenda isimpate Pochettino. Ukiangalia rekodi za Solskjaer katika klabu za Cardiff na Molde usingemuweka katika orodha ya makocha wa juu,” aliongeza Jenas.
 
Hata hivyo, hakuwa chaguo la kwanza mwezi Desemba na nashangaa kwanini klabu haikuchukua maamuzi magumu kubakia katika mpango wake wa awali. Labda ilihofia huenda isimpate Pochettino. Ukiangalia rekodi za Solskjaer katika klabu za Cardiff na Molde usingemuweka katika orodha ya makocha wa juu,” aliongeza Jenas.
 
Jenas ambaye soka lake liliathiriwa na majeraha ya mara kwa mara aliongeza fitina zake kwa Solskjaer akidai mpaka sasa jina lake kama kocha haliwezi kuvutia majina makubwa kusaini Old Trafford tofauti na ilivyo kwa baadhi ya makocha wengine wakubwa England.
 
Back
Top Bottom