Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unaposikia mmoja akianza kusema Machotara na Wahindi si kwao Zanzibar inashangaza. Inabidi umkumbushe tu mambo matatu kwa haraka labda atarudi katika mstari:
Mosi, kwamba mji wa Chake Chake wa awali kabisa ambao hadi mwaka 1914 ulikuwa na nyumba karibu 200 ulijengwa katika ardhi iliyotolewa Wakfu na bwana mmoja wa kiarabu Bwana Nassor bin Khalef mwaka 1825 hata kabla Sultani hajahamia Zanzibar.
 
Katika hali hiyo, Zanzibar inahitaji dhamira ya dhati kabisa ya kuunganishwa. Dhamira ya kuondoa hisia ya kuwa kuna wenye Zanzibar na wengine wapo kwa ihsani ya wenye Zanzibar ambao hawaonekani kuwa na ihsani. Dhamira ya kujenga misingi ya umoja inayoendana na uhalisia uliopo kwamba Wazanzibari ni wamoja.
 
Mwanasheria mkuu wa zamani wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, amesema kwamba licha ya Wazanzibari kuamini kuwa nchi yao inatawaliwa na Tanganyika na kwamba haitendewi haki kwenye Muungano, ukweli ni kuwa tatizo kubwa zaidi limo miongoni mwa Wazanzibari wenyewe, hasa wale waliokabidhiwa madaraka ambao wanaweka mbele maslahi ya vyeo kuliko ya taifa lao la Zanzibar,
 
othman massoud.

Nimefuatilia mjadala juu ya kauli ya Mwalimu wangu, Profesa Palamagamba Kabudi, aliyoitoa Bungeni akiwa Waziri wa Sheria wa Serikali ya Tanzania. Miongoni mwa yanayolalamikiwa sana ni kauli yake juu ya hadhi ya Rais wa Zanzibar, hadhi ya Katiba ya Zanzibar na pia hadhi na mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Yamesemwa mengi, yamesemwa na wengi, si madhumuni yangu kuanza kuyarejea.
 
Kwanza, napenda kutanabahisha wasifu wa Profesa Kabudi. Kwa kadri ninavyomuelewa ni mtu anayeufahamu vya kutosha mfumo wa sheria na katiba wa Zanzibar, historia yake na maendeleo yake.
Anajua vionjo na viroja vya siasa za Zanzibar. Anajua hisia na mtazamo wa umma wa Zanzibar. Lakini anajua pia udhaifu wa waliopo katika nyadhifa mbalimbali Zanzibar kama anavyoujua umakini na umahiri wa baadhi ya watu wa Zanzibar.
Ana faida ya kuijua Zanzibar tokea kwa babu zake. Hata jina lake la Palamagamba amelipata Pemba ambako babu yake aliwahi kufanya kazi ya fundi uashi.
 
Wengi wasiomjua Profesa Kabudi, wanadhani ni mwalimu tu wa Sheria wa Chuo Kikuu ambaye hatimaye ameteuliwa kuwa Waziri. Wanaomjua wanakumbuka kwamba wakati wa vita vya Kagera alikuwa Mwandishi Msaidizi wa Mwalimu Julius Nyerere, kazi yake ikiwa ni kushughulikia utaalamu wa kuandika taarifa za vita. Ni katika waliomshauri Mwalimu Nyerere kuwa taarifa zote za vita ziandikwe katika gazeti la Kiswahili la Serikali na waliobaki wanukuu kutoka katika gazeti hilo.
 
Katika falsafa ya vita hakuna kigeugeu bali kuna kujipanga upya. Kama kugeuka kauli au mbinu yako ni njia ya kushinda vita itakuwaje kigeugeu hicho kiwe na ila??? Binafsi yangu sioni kama katika aliyoyasema Profesa Kabudi lipo jambo jipya ambalo viongozi wetu hawalifahamu kwamba hiyo ndio dhana ya Muungano waliyonayo wengi wa viongozi wa umma wa Tanganyika.
 
Kisiwa cha Latham au kwa jina jengine Fungu Mbaraka (au Fungu Kizimkazi) kipo usawa wa kijiografia wa 6’ 54’ 5 S na 39’ 55’ 45’ E. Masafa kutoka Rasi ya Kizimkazi hadi katika Kisiwa hichi ni maili 36 (kilomita 57.9) na masafa kutoka kusini mwa Dar es Salaam ni maili 37 (kilomita 59.5). Aidha, masafa ya karibu kabisa baina ya kisiwa hicho na Tanzania Bara (sehemu za Kimbiji) ni maili 23 na nusu. Kisiwa hichi kina urefu wa yadi 350 sawa na mita 320 na upana wa yadi 180 sawa na mita 164.5 (kwa vipimo vya mwaka 1898).
 
tuangalie mifano michache tu. Mmoja wa viongozi waliokuwa mstari wa mbele kumlaumu Profesa Kabudi, ndiye aliyetoa pendekezo la kuongeza kifungu kinachosema Zanzibar ni miongoni mwa nchi katika nchi mbili zilizounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa kupitisha mapendekezo ya marekebisho ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar. Pendekezo hilo lilikubaliwa baada ya kueleza matukio kadhaa ya jinsi viongozi wa Serikali ya Muungano wanavyoidhalilisha Zanzibar ndani na kimataifa, akitoa mifano iliyomsibu yeye binafsi nje ya nchi.
 
wakati wa mchakato wa Katiba Inayopendekezwa kule Dodoma, mmoja wa viongozi wakuu wa sasa wa Baraza la Wawakilishi – kwa kushirikiana na wajumbe wenzake wa Kamati ya Uandishi – aliwahi kupeleka mbele ya kikao kilichoongozwa na mmoja wa viongozi wakuu wa Serikali ya sasa hivi, mambo 17 ambayo walihisi yanaibana Zanzibar katika Katiba Inayopendekezwa,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…