Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uhalali wa Rais wa Muungano kwa Upande wa Zanzibar [Ibara ya 89(6)]

Ibara ya 89, Rais wa Jamhuri ya Muungano anaweza kuwa mgombea wa Chama au mgombea binafsi. Chini ya ibara ya 89(6), mgombea urais atatangazwa ameshinda iwapo atapata zaidi ya asilimia hamsini ya kura zilizopigwa. Chini ya Katiba Inayopendekezwa, mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ni makubwa ikiwemo yale ya kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na sehemu.
 
Masharti haya yanazua maswali muhimu yafuatayo:

  1. Kama Zanzibar ni mshirika sawa katika Muungano, kwa nini isiwe na sauti hata kidogo katika kumchagua mtu wanayemkabidhi mamlaka ya utaifa wao;
  2. Iwapo kama Rais wa Muungano na chama chake hawakupata kura hata moja Zanzibar, uhalali wake wa kutekeleza mamlaka makubwa ya kiutawala kwa watu ambao hawakukuchagua unatokana na nini?
  3. Iwapo Zanzibar – ambayo ni mshirika katika Muungano – haikubaliani na usimamizi wa Rais katika masuala yao yaliyopo chini ya Muungano, ina haki gani ya kikatiba au ya kisheria ya kumdhibiti Rais huyo ikiwemo tabia ya Rais huyo kuonyesha dhahiri kuikandamiza Zanzibar?
 
Mamlaka ya BUNGE [Ibara 134]

Ibara ya 134 ndio inayoimaliza kabisa Zanzibar. Ibara hiyo inaeleza utaratibu wa namna 3:

  1. Kwanza, chini ya 134(1)(a)- aya hii inahusu utaratibu wa kupitisha Miswada ya inayohusu ama:
  • Sheria ya mambo yasiyo ya Muungano; au
  • Sheria ya Mambo ya Muungano yaliyomo katika Nyongeza ya Kwanza; au
  • Sheria ya Kubadili Katiba
 
Utaratibu utaotumika ni kwa kupitishwa Mswada huo ikiwa utaungwa mkono na Wabunge walio wengi.

  1. Pili ni ibara ya 134(1)(b) – aya hii inahusu utaratibu wa kupitisha sheria inayohusu ama:
  • Kubadili masharti ya Katiba [ni dhahiri kuwa sharti hili limejirudia kwani ni sawa na sharti la ibara ya 134(1)(a) iliyoelezwa hapo juu];
  • Kubadili masharti ya jambo lililotajwa katika Nyongeza ya Pili ya Katiba [ni mambo mawili 2- kubadili masharti ya Katiba ya Muungano yanayohusu Mambo ya Muungano na kuongeza au kupunguza jambo la Muungano]
Utaratibu ni utakaotumika ni kupitishwa iwapo Mswada huo utaungwa mkono na theluthi mbili ya wabunge wa kila upande.
 
Mambo ya Muungano

Kwa miaka mingi Zanzibar imekuwa ikilalamika katika mambo ya Muungano kwa sababu zifuatazo:

  • Wingi wa mambo ya Muungano [kiasi cha 34 kwa sasa];
  • Kukosa ufafanuzi wa mambo ya Muungano;
  • Mambo ya Muungano kuikosesha Zanzibar nyenzo za kiuchumi
 
Mambo ya Muungano chini ya Katiba inayopendekezwa ni 21. Mambo yote hayana ufanunuzi. Kwa mfano elimu ya juu. Unaposema Elimu ya Juu maana yake ni nini. Ni udhibiti tu au ni pamoja na mitaala, uanzishaji wa taasisi za elimu ya juu au ni pamoja na utoaji wa elimu ya juu. Jambo jengine muhimu lililoingizwa katika Orodha ya mambo ya Muungano bila ya kuwa na hata ufafanuzi ni Mawasiliano.

Kwa hakika katika ulimwengu wa leo mtu anapoinyima nchi au hata uchumi wake haki ya kudhibiti Mawasiliano anakuwa wa ajabu kabisa. Ripoti kadhaa za Benki ya Dunia zimeonyesha mchango wa Mawasiliano katika chumi za nchi na uchumi wa dunia kwa jumla.
 
Louis Armstrong

Ella Fitzgerlard

Nina Simone

Ottis Redding

Ray Charles

Sam Cooke

Aretha Franklin

Diana Rose and the supremes

The Four tops

Al Greene

Barry White

James Brown

Etta James

Michael Jackson

B.B King

Ben E. king

Kool and Gang

Stevie Wonder
 
Aidha, kutokana na maendeleo ya teknolojia na kuunganika kwa teknolojia [covergency of technology] mawasiliano ndio hatma ya nchi zote. Tulipofikia sasa kila kitu kinafanywa kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano, kuanzia miamala ya fedha, usafiri wa teksi na karibuni hata friji lako nyumbani litaweza kuagiza kile kilichopungua ndani ya friji. Unajiuliza hivi waliokubali Katiba Inayopendekezwa walikubali kwa uchu wa kipande cha ndizi tu au kwa sababu ya ugonjwa mbaya zaidi ya huo?
 
Kukosekana kwa ufafanuzi katika Katiba juu ya mambo ya Muungano ndiko kuliko ipelekea Zanzibar ikose haki zake katika Kampuni ya Simu ya Tanzania [TTCL] wakati ilipobinafsishwa pamoja na kwamba Serikali zote mbili zilikubaliana kwa maandishi katika Ripoti ya Muafaka wa Serikali Mbili kwamba haki ya Zanzibar ipatiwe ufumbuzi.
 
Jambo jengine ambalo limeingizwa katika Mambo ya Muungano bila ufafanuzi na linaiangamiza Zanzibar ni katika nyenzo za kiuchumi hasa kodi.

Kwa mfano, Kodi ya mapato ndiyo nyenzo kuu ya kuendesha uchumi wowote wa kisiwa ambacho hakina rasilimali. Kodi ya mapato ndiyo nyenzo ya kuvutia mitaji na ndio nyenzo kupata mapato hata katika rasilimali za nchi.
 
Kura ya Maoni Kubadili Muundo wa Muungano [ibara ya 134(1)(c) na Nyongeza ya Tatu

Katiba Inayopendekezwa imejenga misingi ya dhulma na kukosekana usawa na haki za washirika wa Muungano, jambo ambalo linawafanya watu wa upande mmoja wauchukie Muungano. Kwa upande wa pili, inawalazimisha dhulma hiyo iendelee mpaka pale anayedhulumu atapokubali kubadili dhulma hiyo kwa kupitia kura ya maoni

Hii ni dhulma kubwa dhidi ya Zanzibar. Haiingii akilini kwamba mtu ambaye ana kazi ya kuitetea Zanzibar akubali dhulma hiyo na kutaka kuirasimisha.
 
Profesa Kabudi alianza kwa kuipotosha dhana nzima ya Muungano wa Tanzania pale alipoufananisha na Muungano wa India na Ethiopia.
Kwanza nchi hizo sio za Muungano bali ni za mfumo wa Shirikisho la kugawana mamlaka [federal arrangement].
Pili, shirikisho la nchi hizo halikutokana na muungano wa dola huru (sovereign states).
Tatu, msingi mkuu wa kugawana madaraka baina ya Serikali ya Muungano (Shirikisho) na Serikali shiriki ni kile kiitwacho ugatuzi (devolution).
 
Kwa upande wa Muungano wa Tanzania, kwanza, umetokana na muungano wa dola huru, pili, dola hizo ziliungana kwa mkataba maalum wa kimataifa na tatu, msingi mkubwa wa kugawana madaraka baina ya Serikali ya Muungano na Serikali Shirika ya Zanzibar ni Mkataba wa Muungano, ambao uliweka mfumo wa kuhamisha madaraka (assignment of sovereign powers) kwa msingi kwamba, kwa yale madaraka yasiyohamishiwa katika Muungano, kila upande utakuwa na mamlaka kamili )exclusive powers).
 
Naamini kumbukumbu bado zipo jinsi nilivyofafanua katika kikao cha mawaziri wa pande mbili kule Dodoma juu ya upotoshwaji wa dhana ya Muungano katika Katiba Inayopendekezwa kwa kutaka kuingiza dhana ya devolution badala ya ile ya power assignment and exclusivity iliyoasisiwa na Mkataba wa Muungano, ambao unaeleza kwa ufasaha dhana hii.
 
Hata Mzee Rashid Kawawa alipokuwa akiwasilisha Mswada wa Sheria ya Kuridhia Muungano katika Bunge la Tanganyika, alitumia maneno fasaha sana katika dhana hii. Alisema wazi kuwa chini ya Mkataba wa Muungano, Zanzibar itatoa baadhi ya mambo yake na kuyaweka chini ya usimamizi wa pamoja wa Serikali ya Muungano. Kwa hivyo, chini ya msingi huo, Rais wa Muungano hawezi kuwa na residual power kwa mambo ambayo si ya Muungano kama Profesa Kabudi anavyotaka tuamini.
 
Pili,
Profesa Kabudi anapokataa kwamba hakuna migongano katika katiba mbili, sijui anachukua wadhifa gani katika taaluma ya sheria. Maadili ya taaluma yanahitaji kuheshimu maamuzi ya mahkama za juu za nchi. Mahkama ya Rufaa ya Tanzania katika kesi mbili tofauti – ile ya Seif Sharif vs SMZ [1998] TLR 48 na ile ya Machano na wenzake 17 [SMZ vs ALI [2000]1 EA 216 – imeeleza bayana kwamba ipo migongano ya wazi na ya msingi katika katiba mbili na kushauri hatua zichukuliwe kuondoa migongano hiyo.
 
Tatu, migongano ya kikatiba haiwezi kuondolewa kwa kuisuluhisha kwa kupora madaraka upande mmoja na kuyapeleka upande mwengine. Dawa ya migongano ni kurekebisha katiba. Mifano ipo mingi. Katiba ya Switzerland ya 1874 ilibadilishwa mwaka 1999. Ajenda kubwa iliyopelekea kubadilishwa, pamoja na mambo mengine, ni kutokuwepo bayana jinsi Serikali za Kantoni zitavyoshiriki katika mambo ya nje hasa pale sera na maamuzi ya Serikali ya Muungano yanapoathiri maslahi ya Kantoni. Katiba mpya ya 1999 iliweka bayana na kwa lugha fasaha suala hilo kupitia ibara za 55 na 56.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…