D A E M U S H I N
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 22,665
- 121,102
SUALA LA UMILIKI WA KISIWA CHA LATHAM BAADA YA UJERUMANI KUONDOKA TANGANYIKA
Wakati wa utawala wa Uingereza katika Tanganyika, suala la umiliki wa kisiwa cha Latham halikuwahi kujitokeza. Badala yake, utawala wa Uingereza uliendelea kusisitiza kuwa kisiwa hicho ni mali ya Zanzibar. Mtu mmoja aitwaye Mc Elderry aliiandikia barua Serikali ya Tanganyika akiomba ruhusa ya kuchukua samadi ya ndege kutoka katika kisiwa cha Latham.
Mnamo tarehe 16 Novemba 1934, Sekretariat ya Serikali ya Tanganyika ilimuandikia barua Bw. Mc Elderry kujibu maombi yake. Katika barua hiyo ya majibu, Sekretariat ilieleza kuwa kisiwa cha Latham hakikuwahi kuwa chini ya mamlaka ya Ujerumani.
Aidha, katika kuthibitisha hilo, ilielezwa kuwa hata katika ramani ya Reich’s Kolonialamt iliyochapishwa Berlin mwaka 1908 haikuonyesha kuwa Latham ni sehemu ya mamlaka ya Ujerumani.