Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

5. Iker Casillas – mechi 1,112

Iker Casillas anatajwa kama mmoja wa makipa bora kabisa kuwahi kutokea kwenye historia ya mchezo wa soka. Umri wake wa sasa ni miaka 37 na bado anadaka. Alianza kucheza mwaka 1998 na tangu wakati huo bado yupo kwenye kiwango bora kabisa. Nahodha huyo wa zamani wa Hispania, amebeba mataji mawili ya ubingwa wa Ulaya, Kombe la Dunia mara moja huku akipita kwenye zama bora kabisa katika kikosi cha Real Madrid kabla ya kuhamia FC Porto mwaka 2015.
 
Licha ya umri wake na mazingira aliyopo kwa sasa, kipa huyo bado amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha FC Porto. Hizi ndio timu na mechi alizocheza Casillas hadi sasa, Real Madrid C (26), Real Madrid Castilla (4), Real Madrid (725), FC Porto (149), Hispania (167), Hispania U21 (5), Hispania U20 (2), Hispania U18 (4), Hispania U17 (10), Hispania U16 (19) na Hispania U15 (1).
 
4. Xavi – mechi 1,126

Kiungo wa Kihispaniola, Xavi bado anacheza soka tangu mwaka 1997. Fundi huyo wa mpira kwa sasa anakipiga huko Asia baada ya kutamba kwa muda mrefu kwenye kikosi cha Barcelona. Xavi alikuwa mchezaji muhimu kwenye vikosi vya Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, ambavyo viliweka utawala kwenye soka la Ulaya na duniani kwa ujumla. Kwa sasa anakipiga huko Al Sadd.
 
Hayupo kwenye ubora wake kama zamani, lakini bado miguu yake ina kitu cha msingi inachoweza kukifanya anapokuwa ndani ya uwanja. Hivi ndivyo ilivyo mechi alizocheza Xavi na timu zake hadi kufikia sasa. Barcelona B (61), Barcelona (767), Al Sadd (108), Hispania (133), Hispania U23 (6), Hispania U21 (25), Hispania U20 (6), Hispania U18 (10), Hispania U17 (10).
 
Beki huyo wa kushoto ameichezea Brazil ya wakubwa mechi 125, Brazil U20 (5), kikosi cha Brazil kwenye Olimpiki (23), Uniao Sao Joao (61+), Palmeiras (161), Inter Milan (34), Real Madrid (527), Fenerbahce (104), Corinthians (61), Anzhi Makhachkala (28), Delhi Dynamos (3).
 
Kipa Rogerio Ceni alikuwa mmoja wa wanasoka wachache sana kuwahi kutokea kwenye soka kwa maana kuweka kipaumbele zaidi katika mchezo huo kuliko kufanya mambo mengine. Baada ya kuibukia kwenye soka akiwa katika kikosi cha Sinop, alihamia Sao Paulo ambako alicheza kwa kipindi chote cha maisha yake ya kisoka katika ngazi ya klabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…