KIUNGO mkata umeme, N’Golo Kante amewaondoa hofu mashabiki wa Chelsea kuhusu kinachoelezwa huenda akaachana na timu hiyo kwenda kujiunga na Real Madrid mwishoni mwa msimu huu.
Kiungo huyo Mfaransa amekuwa kwenye kiwango bora kama kawaida yake huko Chelsea licha ya Kocha Maurizio Sarri kumtumia kwenye nafasi ambayo haimwonyeshi ubora wake.
Kiungo huyo Mfaransa amekuwa kwenye kiwango bora kama kawaida yake huko Chelsea licha ya Kocha Maurizio Sarri kumtumia kwenye nafasi ambayo haimwonyeshi ubora wake.
Kante ametumika kwenye kiungo ya juu na Kocha Sarri tangu alipotua Stamford Bridge huku akimtumia Jorginho kwenye kiungo ya kukaba licha ya uhamisho wa Kante kucheza kwenye nafasi hiyo.
Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane ametajwa kuwa ni shabiki mkubwa wa kiungo huyo mkabaji na kinachoelezwa ni kwamba anamfukuzia ili amnase kwenye dirisha lijalo la usajili.
Alipoulizwa kuhusu Real Madrid kumtaka, Kante alisema: “Nipo Chelsea na bado nina mipango hapa, hayo yanayosemwa huko hayana umuhimu. Nipo Chelsea na nimetuliza akili yangu kwenye hilo.”
Chelsea yenyewe haina mashaka juu ya kumbakiza kiungo wake huyo ambaye alisajili dili jipya la miaka mitano kubaki Stamford Bridge Novemba mwaka jana. Kante na mchezaji mwingine anayesakwa na Eden Hazard inaaminika wataisaidia Chelsea kukamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.