Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

 
Theo Walcon (Everton)

MAMBO yamekuwa magumu kwa kiungo wa zamani wa Arsenal, Theo Walcott na klabu yake ya sasa ya Everton inafikiria kumuuza.

Walcott aliyekuwa akiwekwa benchi na Arsene Wenger ameshindwa kutengeneza namba ya kudumu Goodison Park na katika kipindi cha mwezi, na mara ya mwisho alicheza dakika 16 kwenye dabi ya Merseyside Machi 3.

Walcott pia amefunga bao moja tu tangu Agosti kiasi cha kocha wake kushindwa kumwamini kikosini.
 
Saul Niguez (Atletico Madrid)

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amemrahisishia kazi Ole Gunnar Solskjaer wa Manchester United kwenye mbio za kumwania kiungo wa Atletico Madrid, Saul Niguez.

City walioonekana kwenda kasi kwa Sauln na kocha huyo alisema anamtaka mchezaji huyo kama mbadala wa Fernandinho lakini wameghairi na sasa wanamtaka patna wa Niguez, Rodri Hernandezwanaocheza pamoja Atletico.

United kwa sasa wanajiandaa kumnasa Saul kwa ajili ya kuunganisha nguvu na Paul Pogba na Nemanja Matic katika kiungo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…