JUMANNE iliyopita, Mike Dean aliingia kwenye rekodi za kuwa mwamuzi wa kwanza kwenye Ligi Kuu England kuonyesha kadi nyekundu 100, wakati alipomwonyesha beki wa kulia wa Manchester United, Ashley Young.
Wakati hilo la kadi nyekundu 100 za Dean alizoonyesha kwenye Ligi Kuu England ambako amekuwa refa kwa karibu miaka 20, kuna mwamuzi mstaafu, Peter Walton amefichua na kusema kuna nyakati hizo Dean amekuwa akishangilia mabao uwanjani.
Walton, ambaye amestaafu uamuzi wa mechi za soka 2012, amejaribu kumtetea pia Dean akidai kwamba hakuna refa hata mmoja anayekwenda kwenye mechi akiwa na dhamira ya kuonyesha kadi za makusudi.
Refa huyo mstaafu alisema Dean ni mtu mwenye mapenzi makubwa na mchezo wa soka na ndio maana kuna nyakati nyingine amekuwa akishangilia mabao hasa pale linapofungwa akiwa ameruhusu mchezo uendelee kama timu inayoshambulia kuna mchezaji wao amefanyiwa madhambi.
Achana na mambo hayo ya Dean kwamba wakati mwingine amekuwa akishangilia mabao kwenye mechi, ishu ni hizi kadi zake 100 nyekundu alizowaonyesha wanasoka kwenye Ligi Kuu England na hivi ndivyo ilivyokuwa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.