Saul Niguez
Atletico Madrid
KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amemrahisishia kazi Ole Gunnar Solskjaer wa Manchester United kwenye mbio za kumwania kiungo wa Atletico Madrid, Saul Niguez.
City walioonekana kwenda kasi kwa Sauln na kocha huyo alisema anamtaka mchezaji huyo kama mbadala wa Fernandinho lakini wameghairi na sasa wanamtaka patna wa Niguez, Rodri Hernandezwanaocheza pamoja Atletico.
United kwa sasa wanajiandaa kumnasa Saul kwa ajili ya kuunganisha nguvu na Paul Pogba na Nemanja Matic katika kiungo.