Hali ilivyo nchini kwa sasa
Akizungumza wakati wa Jukwaa la Fikra la Mwananchi lililofanyika Juni 28 mwaka jana, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alielezea kwa kina mikakati ya Serikali na mipango ya kisera katika kukabiliana na magonjwa hayo.
Alisema takwimu za WHO mwaka 2010 zinaonyesha endapo hatua mahususi hazitachukuliwa za kupambana na kudhibiti magonjwa hayo ifikapo mwaka 2020, takwimu zitapanda kutoka asilimia 47 mpaka asilimia 60 na kwenye vifo itapanda kutoka asilimia 60 mpaka asilimia 73