Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

4 Victor Ikpeba

Kama ni shabiki wa Nigeria, hii ilikuwa ni penalti zaidi ya ile aliyokosa Baggio. Katika fainali za Mataifa ya Afrika 2000, Nigeria wakiwa wenyeji wenza wakicheza mbele ya mashabiki wao jijini Lagos, walilazika kutoka nyuma mabao 2-0 na kulazimisha sare 2-2 na Cameroon ndipo penalti zilipotumika kuamua mshindi.
 
Wakati wa kupiga penalti ndipo Victor Ikpeba aliyekuwa mwanasoka bora wa Afrika miaka mitatu kabla ya fainali hizo, alikwenda kupiga penalti iliyogonga mwamba. Ikpeba alishika kichwa baada ya tukio hilo na kumshawishi mwamuzi Mtunisia Mourad Daami kuwa mpira huo haukupita mstari, picha ya marudio ilionyesha mpira ulidunda ndani. Basi Cameroon wakatwaa ubingwa.
 
5 David Beckham

Nahodha wa England, David Beckham alikuwa kiongoza wao katika fainali za Euro 2004 katika mchezo war obo fainali dhidi ya Ureno alikwenda kupiga penalti na kupaisha juu na kuishudia England ikitolewa nje.
 
6 Gervinho

Pigo jingine lilitokea mwaka 2012, wakati kizazi cha adhabu cha Ivory Coast kilipofika katika hatua ya penalti kama ilivyokuwa walipochukua ubingwa kwa mara ya kwanza mwaka 1992.

Baada ya Rainford Kalaba kukosa kwa upande wa Zambia ndipo nyota Gervinho alipochukua mpira kwa Ivory Coast kwenda kupiga penalti iliyopaa. Baada kukosa Zambia kutwaa wakatwaa ubingwa kwa kufunga penalti yao ya mwisho.
 
7 Andriy Shevchenko

Katika siku zake, Andriy Shevchenko akiwa moja ya washambuliaji tishio Ulaya akiwa katika kikosi cha AC Milan kilichoongoza 3-0 hadi mapumziko dhidi ya Liverpool katika fainali ya Ligi ya Mabingwa 2005.

Liverpool ilifanikiwa kusawazisha na matokeo kuwa 3-3 ndipo penalti zilipotakiwa kuamua mshindi, Sheva alikosa penalti hiyo kwa kupiga juu na kuiacha Liverpool ikitwaa ubingwa wa kihistoria.
 
8 John Terry

Hiyo ilikuwa nafasi ya nahodha wa Chelsea, John Terry kuibuka shujaa, lakini mambo yakaenda hovyo.

Manchester United na Chelsea walimaliza dakika 120 kwa sare 0-0 katika fainali ya Ligi ya Mabingwa 2008, katika penalti hizo Cristiano Ronaldo alikosa.

Terry akapewa penalti ya mwisho kwenda kupiga endapo angefunga wangetwaa ubingwa, lakini wakati anakwenda kupiga aliteleza na kuipaisha juu. Man Utd ikatwaa ubingwa.
 
9 Lionel Messi

Diego Maradona alitadhalisha kuwa Lionel Messi na wenzake wa kikosi cha Argentina wasirudi nyumbani bila ya ubingwa wa Copa America 2016.

Katika fainali walifanikiwa kucheza dhidi ya Chile baada ya kumalizika kwa dakika 120, ndipo ilipotakiwa kutumika penalti kumpata bingwa. Nahodha Messi alichukua jukumu la kupiga penalti ya kwanza na kukosa. Argentina ikaukosa ubingwa mbele ya Chile.
 
10 Cristiano Ronaldo

Ilikuwa ni shangwe kwa Austria baada ya kushuhudia mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo akikosa penalti na kuingia katika rekodi za mashindano ya Euro 2016.

Ureno ilipata penalti dakika 79, dhidi ya Austria. Ronaldo alipiga penalti hiyo pamoja na kipa Robert Almer kuruka upande tofauti bado nyota huyo alitoa nje.
 
Mshambuliaji huyo alikuwa kinara wa ufungaji alikwenda kupiga penalti ya dakika za mwisho baada ya Luis Suarez kushika mpira, lakini Gyan alikosa na Ghana kutolewa katika hatua ya robo fainali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…