Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

.
FB_IMG_1548263001587.jpeg
 
HUDDERSFIELD na Fulham zimeshuka daraja. Wakati mwingine si wachezaji wote wanaoshuka daraja na timu huwa ni wabovu. Kuna mastaa ambao wanajikuta katika sehemu ambazo si sahihi na katika wakati ambao si sahihi. Wafuatao ni mastaa ambao waliwahi kushuka daraja na timu licha ya ubora wao.
 
Michael Carrick(West Ham 2003)

Mmoja kati ya viungo bora kuwahi kutokea katika soka la Kiingereza. Alitanguliwa tu na kizazi cha akina Paul Scholes, Frank Lampard na Steven Gerrard. Amefanya makubwa katika soka.
 
Katika miaka yake tisa Manchester United, Carrick alitwaa mataji matano ya Ligi Kuu ya England na taji moja la Ulaya. Licha ya mataji haya na ubora wake wa hali ya juu, lakini Carrick aliwahi kuonja machungu ya kushuka Ligi kuu. Mwaka 2003 alishuka na kikosi cha West Ham.
 
Julio Cesar (QPR, 2013)

Kuna nyakati ambazo aliwahi kuwa mmoja kati ya makipa bora duniani. Julio Cesar alicheza katika klabu ya Flamengo ya kwao Brazil kwa miaka saba na kisha miaka saba mingine katika kikosi cha Inter Milan. Ametwaa mataji mengi katika soka la kisasa. Zaidi ya mataji 29 ikiwemo matano ya Serie A ikiwemo yale matatu ya mwaka 2010 kujumlisha na FA ya Italia na Ligi ya Mabingwa chini ya Jose Mourinho.
 
Aliwahi kuchaguliwa mara mbili kuwa kipa bora wa mwaka Italia mbele ya Gigi Buffon.

Aliichezea Brazil mechi 87. Sio wengi wamewahi kupitia sifa hizi. Licha ya sifa zote hizi, lakini mwaka 2013 alishuka na klabu ya QPR katika Ligi kuu ya England.
 
Les Ferdinand

Mfungaji wa nane bora wa muda wote katika historia ya Ligi Kuu ya England. Alifunga mabao 149. Alikuwa katika ubora wake akiwa katika klabu za QPR, Newcastle United na Tottenham. Hata hivyo, licha ya ubora wake na rekodi zake nzuri katika ufungaji hawezi kukwepa ukweli kwamba, alishuka na klabu ya West Ham mwaka 2003 kama ilivyokuwa kwa Michael Carrick. Huzuni.
 
Paolo Di Canio(West Ham 2003)

Paolo Di Canio ni miongoni mwa mastaa waliowahi kucheza katika Ligi Kuu ya England na kupendwa na mashabiki wengi nje ya mashabiki wa timu yake. Di Canio alikuwa na kipaji kikubwa na alikuwa na tabia zilizozua mkanganyiko katika soka. Katika kipindi cha miaka minane England alicheza katika klabu za Sheffield Wednesday, West Ham na Charlton na kujipatia umaarufu mkubwa. Pamoja na umaarufu wake mkubwa katika soka la England, lakini anaungana na Michael Carrick na Les Ferdinand katika kikosi ambacho kiliishusha West Ham mwaka 2003.
 
Michel Salgado(Blackburn Rovers, 2012)

Mmoja kati ya walinzi bora wa pembeni wa muda wote. Michael Salgado ni mkongwe anayeheshimika Real Madrid, baada ya kuichezea timu hiyo ya Satiango Bernabeu kwa miaka 10 huku akicheza zaidi ya mechi ya 350 klabuni hapo. Alitwaa mataji manne ya La Liga na mawili ya Ligi ya mabingwa wa Ulaya. Alicheza pia mechi 53 katika kikosi cha timu ya Taifa ya Hispania. Baadaye aliamua kuonja radha ya Ligi Kuu ya England. Alicheza misimu mitatu katika kikosi cha Blackburn, lakini bahati mbaya kwake akashuka nayo mwaka 2012 na hivyo kuweka rekodi mbovu katika maisha yake ya soka.
 
Mark Viduka(Leeds United, 2004)

Mwamba wa mabao wa Australia. Alitumia miaka tisa katika Ligi Kuu ya England akikipiga katika klabu za Leeds United, Middlesbrough na Newcastle United. Viduka alifunga mabao 92 katika kipindi chake Ligi Kuu ya England huku akiwa na jumla ya mabao 269 katika michuano yote kwa klabu alizochezea na timu yake ya taifa ya Australia.
 
Hata hivyo, maisha yake bora zaidi katika soka yalikuja katika kipindi alichokuwa akichezea Leeds United. Kuna msimu ambao alifunga mabao 17 na mwingine akafunga mabao 20. Hata hivyo, hakutwaa taji lolote katika soka la England ingawa aliichezea Leeds katika kipindi ambacho ilikuwa bora. Huzuni kubwa kwa Viduka ni kwamba, alishuka daraja na Leeds. Na katika siku hiyo hiyo ambayo alishuka daraja na Leeds alipewa kadi nyekundu,
 
Kevin-Prince Boateng (Portsmouth, 2010)

Katika uhamisho wa kushangaza, Kevin-Prince Boateng alikwenda Barcelona msimu huu na kila mtu alibaki na mdomo wazi. Katika siku yake, Boateng ni mmoja kati ya wachezaji bora eneo la kiungo, ambaye anapania kila mechi. Haishangazi kuona amepitia katika klabu nyingi za Ulaya zikiwemo Tottenham, Borussia Dortmund, AC Milan na Schalke
 
Ingawa amezaliwa Ujerumani lakini aliamua kuichezea Ghana wakati mdogo wake, Jerome aliamua kuichezea Ujerumani. Boateng ametwaa mataji mbalimbali ikiwemo lile la Serie A alilotwaa na AC Milan. Lakini, msimu wa 2010-11 alitwajwa katika kikosi bora cha msimu cha Serie A. Hata hivyo, hawezi kukwepa ukweli kwamba alishuka na kikosi cha Portsmouth mwaka 2010 katika Ligi Kuu ya England. Ulikuwa msimu pekee ambao aliichezea timu hiyo.
 
Jermain Defoe (West Ham, 2000

Defoe ni mfungaji bora wa 11 wa muda wote katika historia ya Ligi Kuu ya England. Mashabiki wengi wa soka la Kiingereza wanamkubali Defoe licha ya ukweli kwamba, hajawahi kucheza timu za England kama vile Manchester United, Arsenal, Liverpool au Chelsea. Ubora wake mwingi ulikuja akiwa na kikosi cha Totenham chini ya kocha Harry Redknapp katikati ya miaka ya 2000 na katika msimu wa 2009-10. Defoe pia ni mmoja kati ya wachezaji wachache waliowahi kufunga mabao matano ndani ya mechi moja katika Ligi Kuu ya England. Kitu kikubwa kibaya zaidi kwake katika soka la Kiingereza ni kwamba, alishuka na West Ham mwaka 2003 sambamba na akina Di Canion, Carrick na Ferdinand. Wakati huo alikuwa bwana mdogo.
 
Nwankwu Kanu

Staa wa zamani wa Arsenal na timu ya Taifa ya Nigeria. Ana sifa nyingi kubwa tika soka la Ulaya. Ametwaa ubingwa wa Uholanzi, Ligi Kuu ya England, Ubingwa wa Ulaya, kombe la UEFA, kombe la FA na mengi mengi. Kanu ni mchezaji wa tatu kwa kuingia kama sub uwanjani katika historia ya Ligi Kuu ya England. Alifunga mabao 54 katika msimu 12 aliyocheza Ligi Kuu ya England akiwa na Arsenal, West Brom na Portsmouth. Hata hivyo, katika rekodi zake nyingi nzuri katika soka hawezi kukwepa ukweli kwamba alishuka na klabu ya Portsmouth mwaka 2010 sambamba na Kevin-Prince Boateng.
 
Hivi huyu dada ana nuksi gani aisee anaonekana yuko vizuri ana jielewa.Mungu ampe hitaji lake.
Hana nuksi ni usupa staa tu.
Tangu alivyopata umiss Temeke miaka ile amekuwa ni mtu wa watu kwenye jamii, kiasi baadhi ya hao watu wanaogopa kumtokea.
Ndiyo maana hata kwenye offa yake hapo anasema anataka mtu "Mwelewa"
 
Back
Top Bottom