Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

5. Gareth Bale, Euro 40.2milioni

Gareth Bale alihamia Real Madrid akitokea Tottenham Hotspur karibu miaka sita iliyopita na huko Bernabeu ameshinda mataji mingi kimtindo. Licha ya kwamba ameshindwa kuzivaa buti za Cristiano Ronaldo katika ubora wake msimu huu baada ya Mreno huyo kuachana na Real Madrid, Bale bado anaongoza kwa kulipwa pesa nyingi huko Bernabeu akivuna Euro 40.2 milioni kupitia mishahara yake, bonasi na dili za kibiashara.
 
4. Antoine Griezmann, Euro 44milioni

Antoine Griezmann amekuwa kwenye kikosi cha Atletico Madrid kwa miaka mitano sasa na hivi karibuni tu alisaini dili matata kabisa la pesa ndefu zinazomfanya aendelee kubaki kwenye kikosi hicho kwa muda mrefu. Akiwa ameshashinda pia ubingwa wa Kombe la Dunia 2018 na kikosi cha Ufaransa, staa huyo amejitengeneza sifa kubwa na ndio maana soka inamwingiza kipato cha Euro 44 milioni kupitia mishahara na dili nyingine.
 
3. Neymar, Euro 91.5milioni

Wakati Neymar alipohamia Paris Saint-Germain alitokea Barcelona mwanzoni mwa msimu uliopita, jambo hilo lilimfanya kuwa mwanasoka ghali zaidi katika historia ya mchezo huo baada ya uhamisho wake kuwa karibu Pauni 200 milioni. Sambamba na uhamisho wake kuwa wa pesa nyingi, hata mshahara wake Neymar imekuwa mkubwa pamoja na kubamba dili tamu za kibiashara zinazomfanya avune Euro 91.5 milioni.
 
2. Cristiano Ronaldo, Euro 113milioni

Cristiano Ronaldo ni moja ya wanasoka nyota kabisa dunia na hakika ubora wake ndani ya uwanja umemfanya kuwa mchezaji aliyeshinda mataji kibao. Ronaldo aliushtua ulimwengu wakati alipohama Real Madrid, mahali ambako alibeba mataji manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kwenda kujiunga na Juventus. Dili mpya huko Turin limemfanya Mreno huyo kuwa mmoja wa wakali wanaovuna pesa nyingi, akiweka mfukoni Euro 113 milioni zinazotokana na mishahara na bonasi.
 
1. Lionel Messi, Euro 130 milioni

Mpinzani mkubwa wa Ronaldo ni Lionel Messi kutokana na mchuano wao kwenye kuwania tuzo za Ballon d'Or. Lakini, Messi amemfunika na kumwaacha kwa mbali sana linapokuja suala la kuvuna pesa zinazotokana na mishahara, bonasi na dili za kibiashara. Messi anaweka mfukoni Euro 130 milioni kwa mwaka na kuwa mchezaji anaweka kibindoni mkwanja mrefu licha ya kukosolewa sana huko Argentina kwa kushindwa kuisaidia timu ya taifa kubeba mataji.
 
But when the woman, identified by her surname He, received treatment at Fooyin University Hospital in Taiwan, doctors didn’t find a bacterial infection. While looking at He’s eyes through a microscope, Hung Chi-ting, the hospital’s head of ophthalmology, witnessed something he hadn’t seen before.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…