Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FAIDA ZA KULA NYANYA
Nyanya huwa tunazichukuliwa kama mboga za
majani, ingawa ni kiuhalisia ni tunda.
Nyanya ni chakula kizuri sana. Ni tamu ukila
mbichi katika kachumbari au katika sandwiches,
na zinakuwa na utamu wa aina yake zikiwa
zimepikwa.
 
Nyanya chakula muhimu sana katika mlo wa
watu wa Africa hususan hapa kwetu Tanzania
Nyanya moja inakuwa na calorie 22, gramu 0 za
mafuta, gramu 5 za wanga, gramu 1 za fiber,
gramu 1 ya protini na miligramu 6 za sodium.
Pia inatoa asilimia 40 ya vitamin C
inayoshauriwa kula kwa siku, asilimia 20ya
vitamin A, asilimia 2 ya chumba, na asilimia
moja ya calcium.
 
Zifuatazo ni faida za nyanya:
1.Kinga dhidi ya Saratani.
Tafiti mbalimbali zithibitisha kadiri watu
wanavyokula nyanya nyingi ndivyo inasaidia
kupunguza uwezekano wakupata saratani za
mapafu, tumbo na kizazi. Kitu kinaitwa lycopene
kinachofanya nyanya ionekane nyekundu kwa
rangi inadhaniwa kuwa ndio sababu
inanyoifanyanyanya iwe na uwezo huowa kinga.
Nyanya zilizopikwa ndio zina lycopene nyingi
kuliko nyanya mbichi.
Mchakato wa kuzipika nyanya zinavunja vunja
kuta za chembechembe hai ambako kunasaidia
kutoka kwa lycopene. Ukila nyanya kwa vitu
vyenye mafuta kama mafuta ya olive inasaidia
lycopene kuingia vizuri mwilini.
 
2. Zinalinda Dhidi ya uharibifu wa DNA.
Nyanya uwingi wa antioxidants kama Vitamini C
na Vitamin A. Vitamini hizi zinafanya kazi ya
kulinda DNA dhidi ya kuharibiwa. Pia nyanya
zinaweza kukusaidia kukukinga dhidi ya
magonjwa yanakupata uzeeni kama kisukari.
 
3. Inapunguza Hatari Ya Ugonjwa wa Moyo.
Nyanya zina virutubisho muhimu kama niacin,
folate na vitamin B6 ambazo zinahusika na
kupunguza uwezekano wakupata ugonjwa wa
moyo.
Utafiti mmoja uligundua kuwa wanawake
waliokula nyanya saba mpaka kwa wiki
walikuwa na asilimia 29 pungufu za kupata
ugonjwa wa moyo ukilinganisha na wanawake
waliokula pungufu.
Matokeo ya utafiti huu yalikuwa mazuri zaidi
kwa wale wanawake waliokula nyanya na
vyakula vyenye mafuta.
 
5. Kuzuia Kuvimba.
Utafiti unaonyesha kuwa kunywa glasi moja ya
nyanya kwa siku kunasaidia kupunguza TNF-
alpha kwa asilimia 34 katika damu. TNF-alpha
inasababisha kuvimba mwili.
TNF-alpha nyingi hupatikana kwa watu wenye
magonjwa sugu kama ugonjwa wa moyo,
saratani, osteoporosis na Alzheimer’s.
Kula nyanya nyingi iwezekanavyo ilikupata afya
njema.
Kwan nchi yetu ya Tanzania upatikanaji wa
nyanya ni rahisi sana tena itakuwa vizuri kama
katika kila mlo wako wa siku utakuwa
unatengeneza kachumbari yenye mchanganyiko
wenye nyanya nyingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…