ALHAMISI KUU
Leo ni Alhamisi kuu, tunakimbuka siku ambayo Yesu alikula karamu ya mwisho na wanafunzi wake. Ni siku aliyomfichua msaliti wake. Ni siku ambayo Mimi na wewe yatupasa kutafakari kwa kina dhana ya usaliti katika maisha yetu.
Kwanza, tujitafakari kama tuko sawa katika suala zima la upendo na uaminifu miongoni mwa watu tunaoishi nao?
Pili tujitathimini, je katika maisha yetu tumezunguukwa na akina Yuda (wasaliti) wangapi?
Je, tuna uwezo wa kubaini wasaliti wetu kwenye kazi, ndoa, masomo, mtaani, kanisani, familia nk? Au tunaendelea kula nao katika meza moja bila kuwajua?
Siku ya Leo, omba rehema na neema uweze kumbaini Yuda aliye kwenye maisha yako na umnyoshee kidole kama vile Yesu alivyomuumbua Yuda Iskariote. Omba Mungu wasaliti wako wasiinuke kutoka kwenye maisha yako kama vile ambavyo Yuda aliona aibu ya kuumbuliwa.
Ukimuomba Mungu na kujazwa imani na ujasiri, wasaliti wako hawatashinda bali utaendelea kuwa imara kama ambavyo Yesu alishinda mauti yaliyoanzia kwa Yuda aliyemsaliti.
Ewe Mkristo, omba macho ya rohoni, Utawabaini na kuwaumbua watu wote wanaojifanya wema kwako kama alivyokuwa Yuda kwa Yesu, wakati moyoni wanakuwekea mikakati kamambe ya kukumaliza. Alhamisi Kuu ya leo tangaza maumivu kwa wasaliti wako. Lakini na wewe jitafakari na funga roho ya usaliti.
Amen