Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Safu ile ya washambuliaji watatu matata kwenye kikosi cha Liverpool ndiyo iliyofunga mabao mengi zaidi katika kikosi hicho Anfield na kuwafanya kushindania ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu. Kikosi hicho chenye pointi 85 hadi sasa kimefunga mabao 77 huku mabao hayo yakifungwa na wachezaji 15 tofauti. Chelsea wikiendi iliyopita walikutana na kipigo walipokutana na wababe hao ambao kwa sasa kuwambii kitu kwenye mbio za kuusaka ubingwa wao wa kwanza kwenye Ligi Kuu England. Vinara wao wa mabao ni Roberto Firmino aliyefunga mara 12, Sadio Mane mabao 18 na Mohamed Salah, aliyeweka kwenye kamba mara 19.
 
6. Benfica – mabao 81, wafungaji 14

Benfica na FC Porto wanamenyana jino kwa jino kwenye vita ya kuwania ubingwa wa Ureno baada ya timu hizo zote kulingana pointi, lakini Porto wakiwa na faida ya kuwa na beki nzuri iliyoruhusu mabao 17 tu katika mechi 29 walizocheza.
 
Lakini, Benfica wamekuwa na safu moto kabisa ya kufunga wakiwazidi wenzao mabao 20 baada ya kutikisa nyavu mara 81 kwenye ligi hiyo msimu huu huku mabao yao hayo yakifungwa na wachezaji 14 tofauti. Miongoni mwa wachezaji waliofunga mara nyingi ni Joao Félix, aliyefunga mara 11, Rafa Silva mara 12 na Haris Seferovic, ambaye amefunga mara 19.
 
5. Barcelona – mabao 81, wafungaji 11

Si kitu kinachoshangaza kuona kwamba Lionel Messi ndiye mchezaji aliyehusika kwa asilimia 40 ya mabao ya Barcelona waliyofunga kwenye La Liga msimu huu. Zaidi yay eye na straika Luis Suarez, hakuna mchezaji mwingine kwenye kikosi hicho cha Barcelona mwenye uwezo wa kufikisha tarakimu mbili ya mabao.
 
4. Man City –mabao 86,wafungaji 13

Liverpool na Chelsea ndiyo timu pekee zilizoikomea Manchester City msimu huu. Kikosi hicho ambacho kufunga haijawahi kuwa shida kwao hasa kwa msimu huu wakiwa kwenye mchakamchaka wa kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu England, ina mastaa wawili waliofunga mabao yanayozidi 10 kwenye ligi ngumu kiasi hicho.
 
Kwenye ligi msimu huu wamefunga mabao 86 huku wachezaji 13 tofauti wakihusika kwenye mabao hayo licha ya kwamba Raheem Sterling (17) na Sergio Aguero (19) ndio waliofunga mara nyinbgi zaidi. Lakini, imevuna mabao mengine mengi kutoka kwa mastaa kama Leroy Sane na Gabriel Jesus.
 
Wako pointi sawa na Ajax, kila moja ikiwa na 74, hivyo wanaweza kushindwa kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa. Mabao yake 89 iliyofunga PSV, yamefungwa na wachezaji 14 tofauti, huku waliofunga mara nyingi zaidi ni Gaston Pereiro (10), Steven Bergwijn (13), Hirving Lozano (17) na Luuk de Jong (26).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…