Roma ilihitaji huduma ya kocha Antonio Conte, aliyewahi kuinoa pia Chelsea, lakini wakaamua kumpa kazi Claudio Ranieri kwa muda hadi mwisho wa msimu. Tangu Februari kumekuwa na taarifa hizo za Sarri na kuelezwa kwamba ameshakutana na mabosi wa AS Roma na kwamba wanachosubiri ni Chelsea tu wamfute kazi ili wao wafunguke rasmi.
Fowadi huyo anayelipwa mshahara wa Pauni 505,000 kwa wiki amekuwa na maisha magumu huko Old Trafford tangu alipojiunga Januari mwaka jana akitokea Arsenal.
Amefunga mabao matano tu katika mechi 41 alizoichezea timu hiyo kwenye michuano yote na huenda akafunguliwa mlango wa kutokea mwishoni mwa msimu huu ambapo Juventus wanapiga hesabu za kuinasa saini yake. Kwenye Ligi Kuu England, Sanchez ameanzishwa mara nane tu katika mechi 17 msimu huu.
Katika mechi hizo 17 alizocheza, amefunga bao moja tu na kuasisti mara tatu. Kwa mujibu wa takwimu za Bwin ni kwamba, Sanchez ametumikia dakika 917 kwenye benchi, ikiwa ni sawa na Pauni 5,323 kwa dakika na Pauni 4,881,014 kwa ujumla wake.
Staa wa Liverpool, Daniel Sturridge anashika namba mbili kutokana na kuvuna Pauni 4,646,207 kutokana kutumikia dakika 2,353 kwenye benchi, ikiwa nyingi kuliko mchezaji mwingine yeyote yule kwenye ligi hiyo.