Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Duh [emoji16][emoji16][emoji16]
2e42d80eedb23751287ebe0617d1cb7a.jpeg
 
MAENDELEO YA AFYA YA TUNDU LISSU PATR 2

Sasa kazi kubwa iliyobaki ni kukunja goti na kujifunza kutembea tena. Naomba mniamini nikisema kujifunza kutembea tena, baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa kulala kitandani, ni kazi ngumu sana!!!! Nafikiri sina tofauti sana na mtoto mdogo anayejifunza kupiga hatua zake za kwanza. Lakini pole pole nitafika inshaallah.
Tarehe 14 ya mwezi ujao nitapimwa urefu wa miguu ili nitengenezewe kiatu au soli maalum kwa ajili ya mguu wa kulia.
Kwa sababu ya majeraha makubwa niliyopata, mguu huo ni mfupi kwa sentimita kadhaa. Bila kiatu au soli maalum nitakuwa 'langara' sana na madaktari wamesema hiyo sio sawa sawa.
Kwa kumalizia, sasa nina tarehe ambayo madaktari wangu wamesema nitakuwa 'fiti' kurudi nyumbani.
Msiniambie niiseme kwa wakati huu. Tunahitaji kushauriana na wadau mbali mbali kuhusu tarehe halisi na namna bora zaidi ya kurudi kwangu nyumbani.
Tukumbuke tu kwamba waliotaka kuniua mchana kweupe katikati ya mji wa Dodoma bado wanaitwa 'watu wasiojulikana.' Itabidi tupate 'security guarantees' kutoka kwa wahusika, Serikali ya Magufuli na Jeshi la Polisi, kwamba nitakuwa salama nikirudi.

Kwa hiyo, wakati muafaka utakapofika, hopefully sio mbali sana, nitawaeleza tarehe kamili ya kurudi nyumbani na, kwa mlioko Dar, nitawaomba mniandalie supu ya utumbo wa mbuzi Rose Garden kwa Mzee Assey!!!😋😋😋😋 Wasalaam
 
Back
Top Bottom