Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1075343
 
.MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang amewafuata Mohamed Salah wa Liverpool na Sergio Aguero wa Manchester City katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu cha ufungaji bora Ligi Kuu England.
 
Wachezaji hao kwa sasa wamemtangulia kwa bao moja katika msimamo, lakini Aubameyang alisema hakubali, katika mechi tano zilizosalia lazima atapiga mabao yatakayompa kiatu hicho.
 
Timu nyingi za England kwa sasa zina wastani wa mechi tano kila mmoja kumaliza, huku Liverpool ikiwa kileleni na pointi zake 85 ikifuatiwa na Man City yenye pointi 83. Tottenham na Chelsea ziko nafasi ya nne na tano zikiwa na 67 na 66.
 
Arsenal imebakisha mechi zake na Crystal Palace na Burnley zitakazopigwa Emirates lakini mechi za Wolves, Leicester na Brighton zitakuwa ugenini na strika huyo alisema haoni wa kumzuia kufunga.
 
Jeuri ya Aubameyang imekuja saa chache baada ya kuifungia bao Arsenal na kuifanya iiibuke na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Watford mechi ya Ligi Kuu. Timu hiyo sasa imefikisha pointi 66. Aubameyang mpaka sasa amefikisha mabao 18 msimu huu, akiwa ametanguliwa na Mohamed Salah na Sergio Aguero.
 
Hakuna mchezaji wa Arsenal aliyewahi kutwaa kiatu cha dhahabu tangu enzi za mshambuliaji Robin Van Persie aliyewahi kufikisha mabao 30 msimu wa 2011-12 na kutwaa kiatu hicho na sasa Aubameyang anainyatia rekodi hiyo.
 
Alipoulizwa Gary Neville, mchambuzi wa soka kama itatokea mchezaji huyo atampiku Salah na Aguero, alijibu: ‘Yeah, kwani ajabu ni nini, ana uwezo wa kuwapita.
 
Ninafahamu ni kazi ngumu, lakini nitatwaa taji la ufungaji bora,” alisema. Salah mwenye kiatu cha misimu miwili, alipandisha chati kwa Chelsea wakati Liverpool ilipoishinda mabao 2-0 Uwanja wa Anfield Jumapili na kufikia mabao hayo 18. Aubameyang alisema kuwa mpango uliopo ni kuhakikisha anafunga kila mechi hadi ligi itakapomalizika na ataibuka kinara tu.
 
Back
Top Bottom