Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ushindi huo umeipandisha Everton hadi nafasi ya saba na kufufua matumaini ya kucheza Europa Ligi msimu ujao huku Manchester United ikibaki nafasi ya sita wakiwa nyuma kwa pointi mbili kwa Arsenal inayoshika nafasi ya nne kabla ya mchezo wake wa saa 12:00 jioni leo dhidi ya

Crystal Palace.
 
Liverpool wamesimama, wenzao Manchester City wamekaa. Ni hivi, Liverpool hawakuwa na mechi jana Jumamosi hadi hapo leo Jumapili saa 12:00 jioni watakapocheza na Crystal Palace ugenini, wenzao Man City walijipigia Tottenham na kuketi kileleni kwenye msimamo wa ligi hiyo.
 
Bao la mapema kabisa la Philip Foden lilitosha kuwa Man City ushindi wa 1-0 dhidi ya Spurs huko Etihad na hivyo kuwafanya kufikisha pointi 86 zinazowapandisha hadi kileleni kwenye msimamo wa ligi hiyo, pointi moja zaidi ya Liverpool huku wakiwa wamelingana michezo, kila moja akiwa amecheza mechi 34.
 
Ushindi huo wa Man City unazidi kukoleza moto wa vita ya ubingwa wa ligi hiyo sambamba na Liverpool, ambao kama watashinda ugenini kwa Cardiff City watarudi kileleni licha ya kwamba wao watakuwa mbele kwa mchezo mmoja.
 
Liverpool walikuwa na matumaini ya kuona Man City wanapoteza pointi kwa Spurs, lakini sasa watasubiri kuona itakavyokuwa kwenye mechi dhidi ya Manchester United, lakini wao kwanza itabidi washinde mechi zao.
 
Kwa upande wa Spurs, kipige hicho kinawaweka kwenye wakati mgumu kwelikweli kwani hadi kufika Jumanne wanaweza kujikuta wakiwa kwenye nafasi ya tano kwenye msimamo kutokea kwenye nafasi ya tatu wanayoshika kwa sasa.
 
Kama Arsenal watashinda mchezo wao dhidi ya Crystal Palace leo basi watapanda hadi kwenye nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo, watakuwa na pointi mbili zaidi ya Spurs, sawa na itakavyokuwa kwa Chelsea kama watashinda kesho Jumatatu kwenye mchezo wao dhidi ya Burnley uwanjani Stamford Bridge.
 
Arsenal watakuwa nyumbani Emirates na bila shaka watahitaji kutumia vyema fursa hiyo ya Spurs kuchapwa ili wao kutinga kwenye nafasi ya tatu katika msimamo kuendelea na harakati zao za kufuzu mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
Man United nao wangeweza kuwashusha Spurs hadi kwenye nafasi ya sita kama wangekuwa na uwiano mzuri wa mabao endapo wataibuka na ushindi huko Goodison Park watakapokwenda kumenyana na Everton.
 
Jeshi hilo la Ole Gunnar Solskjaer kama litaibuka na ushindi ugenini kwa Everton litawafanya kufikisha pointi 67 sawa na za Spurs, lakini zitatofautiana kwenye tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.
 
Ligi hiyo kwa sasa imebakiza mechi chache sana kufika mwisho huku vita ya kusaka Top Four ikizidi kunoga zaidi baada ya kuona Spurs waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kuwapo ndani ya timu nne za juu wakipambana na hali yao kufukuzia nafasi hiyo inayotoa fursa ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu ujao.
 
Back
Top Bottom