Inaonekana kwamba watu hawaamini kuwa kuna uwezo wa kuondoa mizigo ya hisia mbaya kwa upesi zaidi. ingawa mazingira yanaonyesha lazima kuwe na badiliko lingine kwanza.
1.Kuwa mkweli, muwazi, kutokana na chanzo cha aibu
Tuingie kwenye mifano ya kanuni. Unapenda kulala sana usiku, lakini unapenda kuamka mapema . kila siku unajikuta umechelewa kuamka, unajisikia vibaya kwa ajili ya hali hio.
Ukitaka kuamka kwa jambo la muhimu siku hio unaweza, lakini mara nyingi kwenye mambo mengine unachelewa kuamka mpaka marafiki zako wanajua kuwa unalala sana.
Hisia hufuata matendo. kama ukifanya bila aibu kujifunza kuamka mapema unaweza kufanya hivyo bila ya kuwaambia rafiki zako. pia jisikie kuwa hukufanya kosa ila ulijitengenezea tabia hio na kwamba una uwezo wa kutengeneza tabia mpya ya kuamka mapema.
Watu wanaweza kukubaliana na wewe kwa kuwa umekuwa mkweli kuhusu tatizo ulilokuwa nao.
Kati ya asilimia 50 ya mahusianon yanakuwa na hisia tofauti, kwa maana kwamba hayo mahusiano ni chanzo cha kuwaza vizuri au vibaya . Wenza wetu na wanafamilia mara nyingi wanazifahamu hizia zetu, na hufahamu namna ya kuzikataa.
Fikiri wakati ambapo mwenza wako anapoleta maumivu yake na kutaka kukuumiza wewe au familia inakusema vibaya kuhusu mwonekano wako, au mwenza wako kukuambia makosa ambayo yalikwisha pita miaka mingi.
Kuna watu hutamani kuwa na malengo mengi, mfano, kukimbia, kujifunza lugha mpya, kutaka kuwa na misuli kama wengine, kununua gari nyingine, kujenga nyumba nyingine.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.