Kuthubutu
Hii ni tabia muhimu sana kwa mjasiriamali,hapa tunazungumzia uwezo na utayari wa kufanya maamuzi ya kuingia katika biashara fulani au mradi fulani huku ukiwa umeondoa nidhamu ya woga. Watu wengi ni waoga wa kuchukua hatua au kuthubutu kuingia katika biashara,mradi n.k,watu wanaogopa hasara, hawajui jinsi ya kuendesha mradi weyewe.