Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sisi binadamu ni viumbe wa kihisia na siyo wa kufikiri kama tunavyofikiri. Msingi wetu wa kwanza katika kufanya maamuzi yoyote yale unaanza na hisia. Labda kuna kitu tunatamani kuwa nacho na hivyo tunasukumwa kuchukua hatua ili kukipata. Au kuna kitu ambacho kinatuumiza na hivyo tunachukua hatua ili kukiondoa.
 
Hisia hizi mbili, tamaa na maumivu ndiyo zinaendesha asilimia 99 ya maamuzi ambayo tunayafanya kila siku. Na mbaya zaidi, huwa tunafanya kwanza maamuzi kwa hisia, kisha baadaye tunajihalalishia kwa kufikiri, kitu ambacho kinafanya tuzidi kujidanganya na kushindwa kufanya maamuzi sahihi.
 
57059896_103761790772857_5306373678154305111_n.jpg
 
Hali hii ya kufanya maamuzi kwa hisia badala ya kufikiri tumeirithi kutoka kwa watangulizi wetu ambao waliishi miaka mingi iliyopita na katika mazingira mabovu sana. Fikiria binadamu ambaye aliishi karne ya tano, ambapo alikuwa akiishi porini na wanyama, kama alikuwa porini na kusikia kishindo asichokielewa, njia pekee ya kupona ilikuwa ni kuchukua hatua haraka, na siyo kuanza kujiuliza kishindo hicho ni cha nini. Katika maisha hayo magumu na mazingira yasiyo salama, kufanya maamuzi kwa hisia kulikuwa na manufaa kwa mwanadamu.
 
Kwa kufanya maamuzi kwa hisia kwenye zama hizi, ni hasara kubwa sana kwetu, wale watu wanaoweza kubonyeza hisia sahihi kwetu, wananufaika sana kupitia sisi. Mfano mzuri ni wafanyabiashara, wanajua bila ya kuibua tamaa au maumivu ndani yako hutanunua wanachouza.
 
Hivyo wanatumia kauli ambazo zitaibua hisia ndani yako, kauli kama; ‘nafasi au bidhaa zimebaki chache, wahi kabla hujakosa’, au ‘kila mtu anatumia kitu hiki, usikubali kupitwa’, zote zinaibua hisia ndani yetu na kutusukuma tuchukue hatua, hata kama kitu hatukihitaji kweli.
 
Mwandishi Robert Green ambaye ametumia muda wake mwingi kujifunza asili na tabia zetu sisi binadamu, ametushirikisha kwa kina sheria kumi na nane za asili ya binadamu kwenye kitabu chake cha LAWS OF HUMAN NATURE.
 
Katika kitabu hiki, sheria ya kwanza ametuonesha jinsi ambavyo hatufanyi maamuzi kwa kina, jinsi tunavyosukumwa na hisia na akatupa hatua tatu za kutuwezesha kutawala hisia zetu na kuweza kufanya maamuzi kwa usahihi.
 
HATUA YA KWANZA; TANBUA UPENDENDELEO ULIONAO.

Kikwazo cha kwanza kwenye kufikiri kwa usahihi na kufanya maamuzi sahihi ni upendeleo ambao tunao. Kila mmoja wetu kuna vitu anapendelea zaidi ya vingine. Na tunapokuwa na upendeleo, huwa tunajihalalishia kile tunachofanya hata kama siyo sahihi.

Hivyo hatua ya kwanza ya kufikiri kwa usahihi ni kutambua upendeleo unaotumia kwenye maamuzi na kuacha kutumia upendeleo huo.
 
Kuna aina mbalimbali za upendeleo ambazo tumekuwa tunazitumia kwenye kufanya maamuzi yetu. Upendeleo huo ni kama;

Upendeleo wa uthibitisho, hapa unatafuta taarifa au ushauri ambao unathibitisha kile unachotaka wewe. Mara nyingi huwa tunakuwa na kitu tunachotaka kufanya, lakini hatuna uhakika, hivyo tunatafuta taarifa au ushauri unaothibitisha kwamba kitu hicho ni sahihi. Na kwa zama hizi za taarifa, hutakosa taarifa inayokubaliana na unachotaka kufanya, hata kama siyo sahihi.
 
Back
Top Bottom