Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Vita ya ubingwa inazihusu timu mbili tu, Liverpool na Man City, lakini ile ya Top Four inahusu vigogo wanne wanaoshindania nafasi mbili, ambao ni Tottenham Hotspur, Chelsea, Arsenal na Manchester United.
 
Mambo ni magumu na Tottenham imejiweka kwenye hasara zaidi ya kutupwa nje ya Top Four licha ya sasa kushika nafasi ya tatu baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa West Ham United jana Jumamosi.
 
Bao la kipindi cha pili la Michail Antonio limechafua hali ya hewa huko kwenye kikosi cha Spurs, ambapo sasa na pointi zao 70, wanaweza kusukumwa nje ya vita hiyo kama wapinzani wake watashinda mechi zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…